August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkurugenzi ATCL kizimbani

Spread the love

DAVID Mattaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuliingizia serikali hasara ya Dola za Marekani 772,402.08, anaandika Faki Sosi.

Akisoma mashtaka Vitalis Thimos, wakili wa serikali mbele ya Respicius Mwijage, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu amesema kuwa, mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo kutokana na matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma.

Tuhuma hizo ni pamoja na kutia saini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na taratibu za zabuni.

Mattaka anadaiwa kuungizia hasara serikali kutokana na hatua yake ya kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo katika Kampuni ya AEROMANTENIMIENTO.

Hasara nyengine ni matumizi mabaya kwa kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo yaliyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Ramadhani Mlinga, Mkurugenzi wa Manunuzi ATCL na Bertha Soka ambaye ni mwanasheria wa shirika. Watendaji hao wanadaiwa kushindwa kuzuia ubadhilfu huo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Machi.

error: Content is protected !!