Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mkulima maarufu Mbeya amuangukia Majaliwa, alizeti yadoda ghalani
Habari Mchanganyiko

Mkulima maarufu Mbeya amuangukia Majaliwa, alizeti yadoda ghalani

Magunia ya Alizeti
Spread the love

 

MKULIMA maarufu wa mazao ya alizeti, mahindi, mpunga pamoja na mazao mengine ya chakula katika mkoa wa Mbeya, Raphael Ndelwa amesema shehena ya magunia 4,000 ya alizeti zimedoda kwenye ghala lake kutokana na Taifa kuamua kuingiza nchini mafuta ghafi, masafi kutoka nje. Anaripoti Paul Kayanda, Mbeya … (endelea).

Kwa sasa asilimia kubwa ya watanzania wanakimbilia kununua mafuta ghafi na safi kutoka nje ya Tanzania wakiamini ni gharama nafuu kuliko bidhaa hiyo inayosindikwa nchini.

Ndelwa ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Raphael Group Ltd. ameiomba Serikali kuwangalia kwa jicho la huruma wakulima waliolima zao hilo la alizeti kwa sababu limelimwa kwa wingi na wakulima.

“Waziri mkuu amekuwa mhamasishaji wa kilimo cha zao la alizeti, ili kulikomboa Taifa naomba mshikilie kama mlivyoshikilia kwenye mchele na mahindi, hizi ni alizeti mimi kama Mtanzania mwenzenu ninakwenda kupata hasara siyo chini ya Sh milioni 200,” amesema mkulima.

Akizungumza na waandishi waliotembelea kiwanda chake cha kuchakata mchele, maghala ya kuhifadhia nafaka pamoja na mashamba darasa yaliyopo eneo la Uyole mkoani Mbeya alisema kabla ya serikali kuruhusu mafuta ghafi na safi yaingizwe nchini, alikuwa na uwezo wa kuuza dumu 10 za mafuta ya alizeti kwa siku.

Raphael Ndelwa

“Ilikuwa ni kuanzia lita 200 mpaka lita 400 lakini kutokana na hali hiyo kwa sasa nauza lita 40 pekee jambo ambalo wakulima tunapata hasara kubwa,” amesema.

Pia ameiomba serikali kutengeneza mfumo ambao kila bidhaa zinazolimwa ndani zisiruhusiwe kutoka nje huku akiwataka watanzania kupenda vya ndani.

Alisema kuwa kwa sasa hata wafanyakazi katika kiwanda cha kusindika mafuta ya kula wamekosa ajira kwa kuwa zao hilo halina soko tena kwa kuwa mafuta hayauziki na kuiomba serikali kupitia mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kunusuru kilimo cha zao hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!