November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkufunzi DSJ afariki dunia

Joyce Mbongo

Spread the love

 

JOYCE Mbongo, aliyekuwa mkufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) nchini Tanzania, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Alhamisi, tarehe 18 Novemba 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini humo alipokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Ibrahim Yamola, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na DSJ imeeleza, kusikitishwa kwao na kifo cha mkufunzi na mtaalamu wa kozi ya Public Relations and Advertising na Entrepreneurship.

“Mchango wake katika jamii ya DSJ, taaluma ya habari, utangazaji, uhusiano kwa umma na matangazo haitasahaulika kwakuwa ilisaidia kila mmoja kwa namna yake,” imeeleza.

“Chuo cha DSJ, wafanyakazi na wanafunzi watamkumbuka daima kwa urafiki, ucheshi, ukarimu, usikivu, ushiriki wa Madam Joyce Mbogo katika matukio mbalimbali hapa DSJ.”

“Mungu ailaze roho ya marehemu Joyce Mbogo, Amina. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, jina Lake Lihimidiwe,” imeeleza taarifa hiyo.

Msiba upo Kimara Suka jijini humo.

error: Content is protected !!