KIUNGO wa klabu ya Simba J,onas Mkude kesho tarehe 5 Juni, 2021 atakwenda kujadiliwa mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, baada ya kuingia tena matatani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezaji huyo ambaye toka Simba ilejee kutoka kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs, hajaonekana mazoezini, huku kocha wake Didier Gomes akidai kuwa na matatizo ya kifamilia.
Licha ya kocha huyo kunena hivyo, ukweli ni kwamba mchezaji huyo alifanya tena kosa la utovu wa nidhamu wakati timu hiyo ikiwa nchini Afrika Kusini.
Akitoa ufafanuzi juu ya swala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Simba, Kamanda Mstaafu Suleiman Kova, alisema kuwa kamati hiyo inakwenda kukutana leo na kujadili suala lake.

“Suala la Mkude limeshafika mezani na tutamjadili tarehe 5 (kesho), sisi kazi yetu ni kupokea malalamiko hata ikiwa mara ya pili na zaidi, akikubali kosa tuna muhukumu akikataa tunaita mashahidi wa upande wa ulalamikaji,” alisema Kamanda Kova.
Aidha kamanda Kova alisema kuwa mchezaji huyo atapewa haki yake ya kujitetea mbele ya kamati hiyo kwa kuwa wanazingatia uweledi katika majukumu yao.
“Tutafuta utaratibu ikiwa pamoja na kumpa haki zake za kujitetea tunafanya yote hayo kwa kuzingatia uweledi,” alisema Kova
Leave a comment