Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo Mkude apiga simu Yanga 
Michezo

Mkude apiga simu Yanga 

Spread the love

 

MARA baada ya kuripotiwa kuwa na matatizo ya kinidhamu na klabu yake wakati walipokuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa nchini Afrika Kusini dhidi ya Kaizer Chiefs kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude ameonekana kupindukia upande wa pili wa wapinzani wao klabu ya Yanga kufanya mawasiliano na moja ya kiongozi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mkude kwa sasa shauri lake juu ya utovu wa nidhamu limefikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Suleiman Kova na kutolewa maamuzi hivi karibuni.

Mtoaji taarifa aliliambia Raia Mwema, kwamba mchezaji huyo alifanya mawasiliano zaidi ya mara tatu na kiungozi wa juu mwandamizi wa klabu ya Yanga na kudai kuwa kama mambo yataenda kombo kwenye klabu yake ya sasa ya Simba yupo tayari kukipiga ndani ya Jangwani.

“Mkude mwenyewe alimpigia simu kiongozi huyo zaidi ya mara tatu na aliongea naye kwa muda mrefu na kumwambia yupo tayari kucheza Yanga kama Simba wakimzingua,” kilisema chanzo hiko.

Aidha chanzo hiko kilendelea kueleza kuwa, kilichobaki kwa sasa mchezaji huyo kusubiri maamuzi ya kamati ya maadili dhidi yake na kuna mpango wa kmshusha timu ya vijana kama sehemu ya adhabu kwa kufanya kosa hilo kwa mara ya pili.

Je ni maamuzi gani ambayo mchezaji huyo atayachukua mara baada ya sakata hilo? soma gazeti lako la Raia Mwema la leo kwa habari zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

error: Content is protected !!