Wakati sakata lake la utovu wa nidhamu likiwa bado kwenye mikono ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, kiungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude, amechukua maamuzi magumu mara baada ya kufuta picha zake zote alizokuwa amevaa jezi ya Simba, kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Kiungo huyoa amesimamishwa na uongozi wa klabu ya Simba, toka timu hiyo iliporejea kutoka nchini Afrika Kusini, kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.
Mkude alichukua maamuzi hayo jana, kwa kuondoka picha zote akiwa ndani ya jezi ya Simba, nakuacha picha tano tu, akiwa kwenye mavazi ya kawaida.
Mchezaji huyo anawafuasi (followers) 425,000 kwenye mtandao huo, na hali hiyo iliyozua sintofahamu juu ya hatma yake ndani ya klabu ya Simba, kutokana na sakata lake linaloendelea hivi karibuni.
Hivi karibuni Kamati ya nidhambu ya klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake kamanda mstaafu Seleman Kova ilitoa mapendekezo kwa uongozi kumpeleka mchezaji huyo Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumfanyia vipimo, kutokana na kufanya makossa yanayojirudia.
Leave a comment