August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkosoaji Kenya apigwa risasi

Spread the love

JACOB Juma, mfanyabiashara mashuhuri jijini Nairobi, Kenya pia mkosoaji katika Serikali ya Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi.

Juma ambaye ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii umekuwa ukizua mjadala, ameuawa jana akielekea kwake.

Taarifa kutoka jijini humo zinasema, Juma alipigwa risasi wakati akielekea nyumbani kwake Mtaa wa Karen saa nne usiku wa kuamkia leo ambapo gari lake lilikutwa na zaidi ya mashimo 10 ya risasi.

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation la Kenya, polisi wanasema, hakuna kilichoibiwa kutoka kwenye gari lake, simu zake mbili na pesa vilipatikana ndani ya gari.

Juma alikuwa mwanakandarasi ambaye pia alihusika katika sekta ya uchimbaji madini. Alikuwa mkurugenzi katika Kampuni ya Erad iliyoshtaki Bodi ya Taifa la Nafaka na Mazao kuhusu kandarasi. Alitaka alipwe jumla ya Sh500m na bodi hiyo.

Agosti mwaka jana, alimshtaki Gavana wa Jiji la Nairobi, Dk. Evans Kidero akitaka akaunti zake za benki zifungiwe kwa tuhuma kwamba alihusika katika ufujaji pesa wa Kampuni ya Sukari ya Mumias Sugar.

Miaka 10 iliyopita, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Juma pia alimshtaki binti wa Rais Mstaafu, Daniel Arap Moi kutokana na kuwa na shamba la ekari 250. Aidha, aliwahi kumshitaki mara mbili William Ruto, Makamu wa Rais wa Kenya.

Amekuwa akikosoa sana Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na ni mmoja wa waliokuwa wakiishinikiza sana kuhusu Sakata la Eurobond.

error: Content is protected !!