August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkongo  kizimbani kwa ‘utakatishaji fedha’

Spread the love

JEAN Bishikwabo (48) raia wa Kongo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa shitaka la kutakatisha fedha kiasi Sh. 14 bilioni, anaandika Faki Sosi.

Mtuhumiwa huyo mkazi wa Kinondoni Biafra, Dar es Salaam amepandishwa kortini leo na kusomewa mashitaka na Diana Mkondo Wakili wa Serikali mbele ya Respecious Mwijage Hakimu wa mahakama hiyo akidaiwa kujipatia fedha hizo kwa udanganyifu.

Katika kesi hiyo, mtu huyo anadaiwa kujifanya ni msambazaji na mnunuzi wa zao la korosho ambapo kati ya Oktaba  2015 na Januari 2016 na kujipatia kiasi cha Sh. 14 bilioni  kwa njia ya udanganyifu kutoka katika Benki ya Biashara ya  Afrika (Commercial Bank Of Africa).

Kutokana mashtaka hayo mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote wala kupewa dhamana kutokana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kewsi zinazohusu utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Mtuhumiwa huyo amerudishwa rumande na kesi hiyo inatarajia kutajwa tena tarehe 25 Agosti mwaka huu.

error: Content is protected !!