June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkewe Jose Chameleone atema nyongo

Jose Chameleone akiwa hospitalini

Spread the love

MKE wa msanii mkongwe Afrika Mashariki, Jose Chameleone, Daniella Atim amewajia juu watu waliosambaza picha za mumewe wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Nakasero nchini Uganda mwishoni mwa wiki. Imeandaliwa na Mwandishi Wetu … (endelea).

Chameleone alikimbizwa hospitali Alhamisi wiki iliyopita baada ya kudaiwa kuwa ameathiriwa na bakteria anayefahamika kwa jina la ‘helicobacter pylori’ anayesababisha vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, baada ya kupatiwa matibabu saa chache baadae aliruhusiwa lakini siku iliyofuata yaani Ijumaa alizidiwa na kurejeshwa tena hospitali ambako alilazwa.

Daniella Atim akiwa na mume wake, Jose Chameleon

Baada ya taarifa za kuugua kwake kusambaa sambamba na picha akiwa amelazwa, baadhi ya vyombo vya habari vilidai msanii huyo anasumbuliwa na maradhi ya figo, maini na kongosho kutokana na matumizi ya pombe kali.

Hata hivyo, mkewe alijibu tuhuma hizo na kudaiwa kuwa mumewe alikuwa ameathiriwa na bakteria.

Pia alieleza kukasirishwa na kitendo cha watu kusambaza picha za mumewe na kudai hali hiyo itaweza kuleta mshtuko kwa wanawe watano.

Mkewe huyo ambaye anaishi Marekani na familia ya Chameleone, pia ameibua maswali kuhusu uhusiano wake na mumewe huyo waliyeishi kwa zaidi ya miaka 13 huku wengi wakidai inawezekana kuwa wameachana na kukubaliana kulea watoto pekee.

error: Content is protected !!