Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkemia Mkuu kuchunguza gongo iliyoua Dar
Habari Mchanganyiko

Mkemia Mkuu kuchunguza gongo iliyoua Dar

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa taarifa kuhusiana na vifo vya watu 10 vinavyodaiwa kutokana na unywaji wa gongo, anaandika Charles William.

Vifo hivyo vilivyotokana na watu hao kunywa gongo ambayo ni pombe ya kienyeji isiyoruhusiwa hapa nchini, viliripotiwa kutokea tarehe 3 na 4 Oktoba mwaka huu katika hospitali ya Tumbi na Mwananyamala huku watu wengine wakifa nyumbani kabla ya kupelekwa hospitali.

Hii ni taarifa kamili ya polisi iliyotolewa leo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam mnamo tarehe 04/10/2017 majira ya saa kumi kamili alfajiri lilipokea taarifa kutoka kwa mwananchi aitwaye MATIGO RAMADHANI (38) mkazi wa Kimara Stop over kuwa tarehe 03/10/2017 majira ya saa kumi na moja jioni ndugu yake aitwaye MALEO RAMADHANI (45) mkazi wa Stop over alirudi nyumbani akilalamika kuumwa tumbo, kuishiwa nguvu na kizunguzungu na kumweleza alikunywa pombe ya kienyeji kwa mama aitwaye  ANOZA.

Alimpeleka Hospitali ya Mwananyamala na baada ya kupata matibabu alirudi naye nyumbani na hatimaye alifariki dunia usiku.

Baada ya muda alijitokeza mtoa taarifa mwingine aitwaye PAULA KISANGILA (53) mkazi wa Stop over alieleza kuwa aliporudi nyumbani kwake kutoka kwenye shughuli zake majira ya saa tano usiku hakumkuta mlinzi wake ajulikanaye kwa jina moja la YONA umri kati ya miaka 20-30 mkazi wa Stop over walijaribu kumtafuta na baadae walimkuta akiwa amefariki nje ya uzio.

Aidha taarifa nyingine zilipatikana kuwa kuna watu wengine saba wamefariki dunia kwa kunywa pombe hiyo ya kienyeji na miili yao ipo katika Hospitali ya Mwananyamala na hospitali ya Tumbi Kibaha ,majina yao ni;

1. MOHAMED ISSA miaka 67, mkazi wa Kimara Saranga
2. KABUGI RASHIDI miaka 64, mkazi wa Kimara Saranga
3. STANSLAUSI JOSEPH miaka 58, mkazi wa Kimara Saranga
4. STEPHEN ISAYA miaka 61, mkazi wa Kimara Saranga
5. MONIKA RUGAILLUKAMU miaka 42, mkazi wa Kimara Saranga
6. ALEX MADEGA miaka 41, mkazi wa Kimara Korogwe
7. HAMISI MBALA miaka 35,mkazi wa Kimara Golani.

8. EKSON NYONI miaka 28, mkazi wa Kimara Stop over Upelelezi wa awali uliweza kubaini kuwa eneo la tukio lililokuwa linauzwa  pombe ya kienyeji ni eneo la Kimara Stop Over na mtu aliyekuwa akiwauzia pombe marehemu hao anajulikana kwa jina la mama ANOZA.

Katika eneo la tukio ziliokotwa chupa tatu za ujazo wa lita moja zikiwa zimejazwa pombe inayodhaniwa kuwa ni pombe ya moshi (gongo).

Vielelezo vyote vinapelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ikiwa ni pamoja na miili ya watu waliokufa ili kufanyiwa uchunguzi na kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo, huku msako mkali ukiendelea kufanyika ili kumkamata mtuhumiwa huyo aliyewauzia pombe kwa hatua za kisheria.

LAZARO MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!