Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mkemia Mkuu atambua miili 50 ajali ya Moro
Habari Mchanganyiko

Mkemia Mkuu atambua miili 50 ajali ya Moro

Lori la mafuta likiteketea kwa moto na kusababisha baadhi ya watu kuungua moto
Spread the love

OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutambua miili 50 kati ya 69 ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya moto wa lori la mafuta mkoani Morogoro.  Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 20 Agosti 2019 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu wakati akizungumzia ziara ya Rais John Magufuli katika ofisi hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo, Rais Magufuli ametoa wito kwa ndugu kujitokeza ili wachukuliwe sampuli zao kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao mahala ilipozikwa.

Aidha, Rais Magufuli ameitaka ofisi hiyo kuendelea kutoa taarifa kwa umma ili ziwafikie walengwa kitendo kitakachosaidia kupata ndugu wa miili 19 iliyobakia.

“Wale wengine kama alivyotoa wito  kiongozo wenu basi kama kuna ndugu wanaweza kuwa tayari wapimwe, ili pawepo ‘comparison’ ya marehemu wachache waliobakia. Mmefanya kazi kubwa sana na hizi taarifa mzitoe mapema mzitangaze sababu itasaidia ndugu wa marehemu kupimwa,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewaomba Watanzania kuwaombea kwa Mungu majeruhi wa ajali hiyo wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ili wapone haraka na waungane na familia zao.

“Lakini wale walioko kule tuendelee kuwaombea Mungu awasaidie, kikubwa ninachotaka kusema ni kwamba ofisi yenu ya mkemia mkuu na ninyi wakemia mmefanya kazi kubwa sana ninawapongeza sana,” amesema Rais Magufuli.

Ajali ya moto wa lori la mafuta ilitokea tarehe 10 Agosti mwaka huu mkoani Morogoro, ambapo mpaka sasa imepoteza maisha ya watu zaidi ya 90.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!