May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mke wa rais aukataa mshahara kukwepa gubu la wananchi

Rebecca Akufo-Ado, mke wa Rais wa Ghana, Nana Akufo-Ado

Spread the love

 

REBECCA Akufo-Ado, mke wa Rais wa Ghana, Nana Akufo-Ado, amegoma kupokea mshahara wa Dola za Marekani 3,500 (Sh. 8.1 milioni) kila mwezi, ili kukwepa maneno ya wananchi wanaomtuhumu fisadi, kutokana na kulipwa fedha nyingi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Rebecca amechukua hatua hiyo hivi karibuni, baada ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa nchi hiyo, dhidi ya kiwango cha fedha anazolipwa kwa kutumia cheo cha mke wa rais, kuzidi tangu mume wake alipoingia madarakani 2017.

2019, Bunge la Ghana lilipendekeza mishahara ya wake wa rais na makamu wa rais wa nchi hiyo, iwe dola 3,500. Wiki iliyopita wabunge wa nchi hiyo walipitisha mapendekezo hayo.

Mbali na kutangaza kususia mshahara huo, Rebecca ameahidi kurejesha dola 151,618 (Sh. 351.6 milioni), alizopewa kama marupurupu, tangu mume wake awe Rais wa Ghana.

Rebecca na mumewe wake Rais wa Ghana Nana Akufo-Ado

“Nimeamua kurudisha fedha zote nilizopewa kama marupurupu, dola 151,618,” amesema Rebecca kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa umma.

Mwanamama huyo amelaani tuhuma zinazotolewa na wananchi dhidi yake, akisema kwamba hakuomba kulipwa mshahara na marupurupu hayo, bali stahiki hizo huzipata kutokana na wadhifa wake.

Amesema ameamua kurejesha fedha hizo, ili kukwepa maoni mabaya yanayotolewa dhidi yake kutoka kwa wananchi, yanayomtuhumu kuwa mbinafsi, fisadi na mtu asiyejali maslahi ya raia wa Ghana.

error: Content is protected !!