Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mke wa Mwandishi Kibiki amtafuta JPM
Habari Mchanganyiko

Mke wa Mwandishi Kibiki amtafuta JPM

Rais John Magufuli picha kubwa. Picha ndogo kulia ni Tobina Kibiki, mke wa mwandishi Emmanuel Kibiki (picha ndogo kushoto)
Spread the love

Tobina Emmanuel, ambaye ni Mkewe Emmanuel Kibiki yule mwandishi wa habari wa Iringa, Makambako, aliyevamiwa usiku wa manane hivi karibuni, amewaomba waandishi kusaidia kufikisha kilio chake kwa Rais Magufuli kuhusu ukatili unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya mumewe na familia yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tobina anasema kuwa, leo asubuhi, akiwa ameambatana na mumewe waliripoti kituo cha polisi Makambako. Kisha wakapelekwa Njombe kwa ajili ya kusomewa mashtaka mahakamani.

Walikaa nje ya mahakama mpaka saa tisa mchana mahakama ilipofunga. Polisi aliyewasindikiza akawaambia kuwa kesi ya Mbiki haijasomwa kwa kuwa hati ya mashtaka ilikosewa.

Hivyo, polisi wakaamua kwamba Kibiki atawekwa rumande mpaka kesho atakapopelekwa mahakmani tena. Tobina anasema kuwa, mpaka sasa mumewe hajaambiwa ni kosa gani linamkabili.

Hivyo, Emmanuel Kibiki amelala mahabusi Njombe, na mkewe Tobina amerudi Makambako kwa ajili ya kukusanya nauli kwa ajili ya safari ya kesho na wadhamini wa mumewe.

“Huu ni ukatili wa kiuchumi wenye lengo la kuisambaratisha familia yangu. Nawaomba waandishi mnifikishiue kilio change kwa Rais Magufuli. Nataka nijue kama ndiye anawatuma hawa watu,” anasema Tobina.

Itakumbukwa kwamba, mnamo usiku wa a tarehe 22 Februari 2018, Tobina Emmanuel, maarufu kama Mama Irene, ambaye ni mkazi wa Makambako Mjini katika eneo la Mwembetogwa, mkoani Njombe, alivigutusha vyombo vya habari.

Usiku huo mzima, alikuwa anapiga simu kwenye vyombo vya habari kutoa taarifa za kuvamiwa na kukamatwa kwa mumewe Kibiki.

Kituo cha luninga cha EATV ni miongoni mwa vyombo vilivyopokea taarifa hizo na kuelekeza macho yake huko usiku huo. Akiongea na EATV, Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu, aliripotiwa kusema kuwa, mpaka muda huo, Jeshi la Polisi lilikuwa halijamkamata mwandishi huyo. Akadai kwamba, huenda amekamatwa na taasisi nyingine zinazohusika na ulinzi na usalama.

Mahojiano yalikwisha na polisi wakamwambia awe anaripoti kituoni kila Ijumaa. Tangu wakati huo amekuwa anafanya hivyo mpaka Ijumaa iliyopita alipoambiwa kuwa ajiandae ili akapelekwe mahakamani jumatatu ya leo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!