Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Mke wa Mrema huyu hapa, aanika utajiri wake, asema hajafuata mali
HabariTangulizi

Mke wa Mrema huyu hapa, aanika utajiri wake, asema hajafuata mali

Spread the love

DOREEN Kimbi, mke wa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Augustino Lyatonga Mrema amesema umri baina yake na mumewe mwenye miaka 77 si tatizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Amesema hayo muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha TLP leo Alhamisi, tarehe 24 Machi 2022, katika Kanisa Katoliki Parokia Uomboni, Marangu mkoani Kilimamnjaro.

Mrema amefunga ndoa hiyo baada ya mke wake wa kwanza, Rose kufariki dunia tarehe 21 Septemba 2021.

“Najisikia furaha. Leo ni siku nzuri na ni siku ya kukumbukwa maisha yangu yote,” amesema Doreen.

Alipoulizwa alikuwa anatarajia kuja kuolewa na mwanasiasa maarufu, Doreen amesema, “kila kitu kinapangwa na Mungu na sikutarajia kama nitakuja kuolewa na mtu maarufu.”

Kuhusu maneno yaliyokuwa yanazungumzwa mitandaoni hivi karibuni na picha kuzunguka zikielezea mchumba wa Mrema, Doreen amesema, hakuwa yeye na wala haikuwa inamsumbua ila ilikuwa inampa furaha.

“Unajua ukiwa kwenye hali kama tuliyokuwa nayo, mimi si mtu wa mitandao, sikuwahi kufikiria na nilijua ni harusi ya kawaida lakini yeye alikuwa anaogopa kwamba nikiona kinachoendelea nitakata tamaa, lakini mimi nilikuwa na msimamo,” amesema.

Huku wakitabasamu kwa furaha, Doreen ameelezea kwa nini aliamua kutoka nyumbani akiwa amejifunika nguo akisema, “mimi si mtu wa mitandao, sasa kwa kuwa watu walikuwa wengi, kamera kibao na kwa kuwa nami nina maisha yangu, niliamua kutoka vile nimejifunika na kwa kuwa sikutaka kuonekana.”

“Picha imetoka mitandaoni hadi nilivyotaka na mimi sikuwa nimejiandaa kwa harusi kubwa, tumepanga tuwe na harusi ya kawaida na siyo kwamba sina hela hapana, nimemua kutoka tu hivi,” amesema.

Akizungumzia ukaribu wake na mume wake, Doreen amesema “mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi mimi. Katika kipindi cha uchumba nimemuweka hivi kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata. Kwa sasa amebadilika na sitarajii kubadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza zaidi, nataka hadi awe kijana.”

Akiwajibu wale wote wanaohoji kwamba amekwenda kufuata mali, Doreen amesema “mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake.”

“Doreen ni mwanamke wa shoka, mpambanaji, siyo wale wa kupaka rangi na kucha ndefu, napenda kuchapa kazi, napenda kujisimamia na napenda kuwasaidia wanawake wenzangu,” amejinasibu.

“Doreen ni dada wa kawaida kabisa kwenye jamii, siyo mwanamke wa mitandaoni, siyo mwanamke anayejua disco, siyo mwanamke anayependa pombe ni mwanamke wa kawaida,” amesema.

Kipi anatamani kukiona kwenye maisha yao mapya, Doreen amesema “natamani kwanza yeye awe katika afya njema siku zote, tuwe katika mstari wa mbele kumtumikia Mungu, umri wake siuoni sana, kwani umri ni namba na yeye na mimi mapokeo yetu hayakuangalia umri ila napaswa kum-take care kwani mimi bado kijana.”

Wamekaa katika uchumba kwa muda gani, Doreen amejibu swali hilo akisema, “
alivyoniona, akanitafuta, tukaongea na haikuwa serious sana na kipindi kile alikuwa anaumwa, nika ‘take care’ na nikajiona naweza kuwa msaada kwake na yeye akawa mwalimu mzuri kwangu, ananielekeza na kunipa njia nzuri ambavyo kumbe naweza kutoka hapa nilipo na kufanya zaidi na hiyo ikawa safari yetu hadi leo.”

Mara baada ya kumaliza kufunga ndoa, Mrema na mke wake wamerejea nyumbani kwake katika kijiji cha Kiraracha- Marangu mkoani Kilimanjaro ambapo kuna shughuli ndogo ikihusisha vinywaji na pombe aina ya mbege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

error: Content is protected !!