September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mke wa mbunge akutwa na Corona

Spread the love

MWANDISHI wa habari wa Sauti ya Ujerumani (DW), anayefanyia shughuli zake Visiwani Zanzibar, Salma Said, amethibitika kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona – Covid 19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akiandika katika ukurasa wake wa twitter, Salma amesema, “nimefanyiwa vipimo na wataalamu wa afya na majibu yaliyokuja leo (jana Jumanne), ni kwamba nimeambukizwa virusi vya Corona.”

Salma, ni mke wa mbunge wa Mwanakwerekwe, Unguja, Ally Salim Khamis, na ambaye amekiri kuwa mke wake huyo, ni amepatwa na maambukizi.

Hata hivyo, Salma anasema, “I’am very comfortable na sina wasiwasi kwa sababu, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona yenyewe.”

Anasema, “tupambane na ugonjwa huu, tutashinda kwa uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu.”

Kwa sasa, Salma amehifadhiwaa kwenye eneo maalum lililotengwa na serikali lililopo huko Kidimni, mkoa wa Kaskazini Unguja kwa matibabu zaidi.

Akiandika kwa marafiki zake na wabunge wenzake wa Bunge la Muungano, Ally Khamis anasema, “ni kweli mke wangu amepata huu ugonjwa. Alianza kuwa na dalili siku 4 zilizopita.”

Anasema, anaendelea kumshukuru Mungu kwa kumpa uwezo wa kuchukuwa tahadhari zote kukabiliana na ugonjwa huo hatari sana. 

Anasema, “baada ya kuona dalili hizo, mwenyewe (Salma) alipiga simu kwa wahusika akielezea hali yake, na alipewa maelekezo na Jumapili iliyopita alichukuliwa vipimo na leo (jana) ameelezwa kuwa amepatikana akiwa na virus vya corona.”

Kauli ya mbunge huyo ilikuja muda mfupi baada ya kuripotiwa kwa taarifa hiyo, huku baadhi ya wabunge wakionekana kuwa na hofu ya maambukizi hayo kuingia bungeni.

Lakini Ally ameeleza kwa kirefu historia ya safari yake tangu kuanza kuripotiwa kuwapo kwa maambukizi hayo ulimwenguni.

Amesema, “…niwatowe hofu ndugu zangu mimi nipo Dodoma tokea tarehe moja Machi. Sijawahi kuondoka kwenda kokote.”

Anasema, mimi ni kiongozi wa wananchi. Nafahamu  umuhimu wa kujikinga na maradhi haya pamoja na kuwakinga wenzangu. Siwezi kwa vyovyote vile, kufanya aina yoyote ya udanganyifu ili kuwasababishia wengine matatizo.”

Mpaka jana serikali ilitangaza watu takribani 56 walikuwa wameambukizwa na virusi hivyo wakiwamo wagonjwa wapya wanane.

Kufuatia kugongezeka kwa maambukizi hayo kwa kasi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alitangaza kufutwa kwa sherehe za wafanyakazi maarufu kama Mei Mosi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha, shule zote za msingi, sekondari na elimu ya juu zitaendelea kufungwa hadi hapo serikali inasema, “itakapotangazwa vinginevyo.”

Taarifa ya wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imeeleza kuwa wagonjwa wote wapya, ni Watanzania.

Amesema, serikali inaendelea kufuatilia watu waliokaribu na wagonjwa hao na inaendelea kuwataka wananchi kuepuka misongamano.

error: Content is protected !!