October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mke wa Kabendera akimbia nyumba

Spread the love

LOY Kabendera, mke wa Erick Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi, anayeshikiliwa katika gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, ametoweka kwa hofu ya maisha yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), leo tarehe 8 Januari 2019, watoto wa Kabendera wamechukuliwa na ndugu zao.

Kabendera na familia yake, wamekuwa wakiishi Mbweni iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni. Mdee amesema, sababu ya Loy kukimbia na kutelekeza nyumba, ni kuhofia usalama wake.

Akizungumza na wanahabari, Mdee aliyejitambulisha kuwa jirani wa Kabendera, amesema mke wa mwanahabari huyo amekimbia kusikojulikana.

“Sisi BAWACHA tumeamua kama mbwai na iwe mbwai, na tumemaanisha. Sababu ifike mahali tuonee huruma, mkikumbuka Mama Kabendera siku kadhaa kabla hajafa, alinukuliwa akimwambia rais, huyu mtoto uliyemuweka ndani ndio ananifanya niwe na uhai,” ameeleza Mdee na kuongeza;

“Kabendera ni jirani yangu Mbweni, familia imehamishwa, watoto haijulikani wanasomeshwa na nani. Mke wake kakimbia, hajui anakamatwa lini.”

Dada wa Kabendera, Prisca Kabendera alipotafutwa na MwanaHALISI Online kuzungumzia alipo mke na familia ya kaka yake (Kabendera), hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

“Siwezi kuliongelea suala hilo na sijui…, tunataka kumlinda yeye na watoto,” amesisitiza Prisca.

Kabendera anashikiliwa kwa zaidi ya miezi mitano sasa, anatuhumiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha, kukwe pakodi na kushirikiana na magenge ya kihalifu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

error: Content is protected !!