April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mke ashirkiana na mtoto kumuua mumewe

Spread the love

MWANAUME mmoja, Boniphace Agustino (46) mkazi wa Chamwino, Morogoro ameuawa na watu watatu akiwemo mke wake na mwanae kwa kumpiga kitu kizito kichwani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Wakizungumzia tukio hilo majirani walioshuhudia tukio hilo akiwemo Mariam Mohammed walidai kuwa tarehe 28 Mei, 2019, majira ya saa nane mchana walisikia vishindo na kelele kiasi kutoka kwa mwanaume huyo akiomba msaada na kudai kuwa mke wake anataka kumuua huku wakiwa chumbani kwao.

Mariam alisema, awali mwanaume huyo alikuwa na ugomvi na mke wake  jambo ambalo ndugu walilisuluhisha lakini wanashangazwa kuona mwanamke huyo akishirikiana na mtoto wake wamefikia hatua ya kufanya mauaji hayo.

Alidai kuwa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Neema Godfrey alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Salum ambaye alikuwa mpangaji wake katika nyumba waliyokuwa wakiishi na mume wake huku pia mwanaume huyo akiwa na mahusiano ya kimapenzi na binti yake aliyefahamika kwa jina la Alphocina Boniphace.

Pia ndugu wa Marehemu, Revina Makundi ambaye alisema, kaka yake huyo na mkewe walikuwa na ugomvi kila mara ambao yeye alikuwa akiusuruhisha juu ya marehemu kukiri kumbaka binti yake wakati akiwa mdogo kwa imani za kishirikina na walisuruhisha na ugomvi ukaisha ambapo akashangazwa na mauaji hayo ya sasa.

Aidha Makundi alisema, pia wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kimapenzi baada ya mpangaji wao kutembea na mke wa marehemu huyo na binti yake ambapo marehemu huyo alimfukuza mpangaji huyo na baadae alirudi.  

Naye mtendaji wa Kata Chamwino, Bright Sospeter alisema, majira ya Saa kumi jioni alisikia watu wakieleza tukio hilo huku wakiwa na hisia za  kutokea mauaji ndipo walijumuika na viongozi wengine na walipofika eneo la tukio na kumuhoji mwanamke ambaye ni mkewe, alisema, mumewe alirukwa na akili mchana na ndio maana alisema anauawa na muda huo wakati anaulizwa hakuwepo.

Sospeter alisema, walipoingia ndani na kumkuta binti walimuuliza akasema baba yake alienda kwa Ustadh kuombewa hivyo hayupo jambo lililowafanya walazimike kupekua nyumba nzima na ndipo walipokuta baba huyo akiwa tayari kashafariki dunia akiwa chooni huku pembeni yake kukiwa na mchi pamoja na damu sakafuni.

Naye Kamanda wa Polisi Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi ambao ni Neema Godfrey (41) Mkazi wa Chamwino, Alponcina Boniface (19) na mtu mwingine ambaye hakuweza kumtaja kwa sababu za kiuchunguzi.

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa alisema, inadaiwa kuwa mpangaji aliyekuwa amehamishwa alihusika baada ya kuingia ndani akiwa amevaa vazi aina ya dela hadi usoni na baadae kutoroka ambapo amewataka wananchi wa mkoa wa Morogoro hususan wakazi wa Kata ya Chamwino kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kufanikisha mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo anapatikana.

MWISHO…

error: Content is protected !!