Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkapa aisisimua CUF, Prof. Lipumba amuita
Habari za Siasa

Mkapa aisisimua CUF, Prof. Lipumba amuita

Prof. Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

BARAZA Kuu la Uongozi wa Taifa la CUF, limeeleza kuguswa na yaliyomo ndani ya kitabu cha Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa ‘Maisha Yangu, Kusudio Langu.’ Anaripoti Martini Kamote … (endelea).

Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho – Taifa ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Novemba 2019, wakati akiwasilisha maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho.

“Baraza Kuu limeguswa na yaliyomo ndani ya kitabu cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin WIlliam Mkapa ikiwemo uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi pia kusononeshwa na mauaji ya tarehe 26-27 Januari 2001,” amesema.

Januari 2001, yalifanyika mauaji wakati wa maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa CUF, kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2000 visiwani Zanzibar.

Prof. Lipumba mesema, Baraza Kuu linamtaka Rais Mkapa kuungana na na CUF, ili kuhimiza utekelezwaji wa mapendekezo ya tume ya Brigedia Jenerali Mbita, ikiwemo kuwalipa fidia waathirika wa matukio ya Januari 2001.

“Rais Mkapa aliunda tume iliyoongozwa na Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita, tume ilitoa taarifa na katika mapendekezo yake, ni pamoja na waathirika wa tukio la tarehe 26 na 27 Januari walipwe fidia.

“Nakumbuka hata mimi niliitwa na jopo la madaktari, kutazama maumivu niliyoyapata lakini toka wamefanya hivyo, bado sijapata taarifa yoyote,” amesema.

Mwenyekiti huyo wa CUF, amekumbushia saa yake aliyodai kuporwa wakati wa dhahama hiyo.

“Saa yangu iliporwa na polisi. IGP atazame tazame kwenye kambi kama ipo aweze kinirudishia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!