Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mkandarasi aliyepewa kazi TPA ‘apiga cha juu’ bilioni 64
Habari MchanganyikoTangulizi

Mkandarasi aliyepewa kazi TPA ‘apiga cha juu’ bilioni 64

Spread the love

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini mkandarasi aliyepewa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika bandari ya Tanga na kulipwa Sh bilioni 104.92, aligawa kazi hiyo kwa mkandarasi mbia na kumlipa Sh bilioni 40.62. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

‘Mkandarasi mkuu’ ambaye hakutajwa jina katika ripoti ya uchunguzi wa CAG, Charles Kichere, alipewa kazi hiyo na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 3 Agosti, 2019 hadi Agosti 2020, alipiga cha juu Sh bilioni 64.30.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma jana tarehe 12 Aprili, 2022 na Kichere imesema TPA iliingia mkataba na “Mkandarasi Mkuu” wa shilingi bilioni 172.36 kwa ajili ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika bandari ya Tanga.

Pia kufanya tathmini ya athari za kimazingira, na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari.

“Kwa kulingana na mkataba, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni shilingi bilioni 104.92 (asilimia 60 ya bei yote ya mkataba).

“Hata hivyo, mnamo tarehe 1 Agosti 2019, “Mkandarasi Mkuu” iliingia makubaliano na “Mkandarasi Mbia” kwa ajili ya kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli kwa bei ya mkataba dola za marekani milioni 18.15 sawa na shilingi bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa TPA,” amesema.

Amesema ‘Mkandarasi Mkuu’ aliingia mkataba na ‘Mkandarasi Mbia’ hata kabla ya kusaini mkataba wake na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Amesema kuingia mkataba bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari ilikuwa ni kinyume na Kifungu Kidogo cha 4.4 cha Masharti ya Jumla ya Mkataba kati ya Mamlaka ya Bandari na Mkandarasi Mkuu.

“Kifungu hicho kinaizuia Mkandarasi Mkuu kutoa sehemu ya kazi kwa Mkandarasi mwingine, na ikiwa kunauhitaji wa kutoa kazi kwa Kampuni nyingine kutekeleza kazi zilizoko kwenye mkataba, Mkandarasi Mkuu anapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari siku 28 kabla ya kutoa kazi hiyo,” amesema.

Aidha, amebaini jumla ya malipo yaliyolipwa kwa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli yalikuwa dola za Marekani milioni 18.22 sawa na shilingi bilioni 40.62, kiasi hiki, pia, kinajumuisha malipo ya dola za marekani 73,824 sawa na shilingi milioni 164.55 kwa huduma za wakala wa meli kwa “Mkandarasi mbia”.

“Ulinganifu wa kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu shillingi bilioni 104.92 na kiasi alicholipwa na “Mkandarasi mbia” shilingi bilioni 40.62 inaonesha kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu kimezidi kiasi halisi kilichotumika kufanya malipo ya kazi hiyo kwa shilingi bilioni 64.30.

“Ninapendekeza TPA na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuchukua hatua kutokana na udanganyifu wa bei uliofanywa na Mkandarasi Mkuu pamoja na maofisa waliopaswa kufanya tafiti za gharama ili kujua makisio halisi ya bei kabla ya kuingia Mkataba na mkandarasi,” amesema.

1 Comment

  • Je hatua za kisheria zitachukuliwa au ni danganya toto tu kwa maneno matamu? Kila mwaka hadisi ni hiyo hiyo. Hebu tuone kama Mama atasema lolote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!