Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkakati wa kutokomeza ukatili wa watoto waiva
Habari Mchanganyiko

Mkakati wa kutokomeza ukatili wa watoto waiva

Watoto waishio kwenye mazingira magumu
Spread the love

SERIKALI imesema kuwa inaandaa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (2017/18-2121/22) ambao miongoni mwa shabaha zake ni kuhakikisha watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwemo watoto na kufanya kazi mitaani wanapata huduma stahiki. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka bungeni Jijini Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile, alipokuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum Aisha Rosse Matembe (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali ina mpango gani wa kuanzisha kampeini ya kitaifa kukabiliana na tatizo hilo kwa nchi nzima ikiwemo kuwaweka kwenye vituo maalum na kuwapatia huduma za msingi.

Pia alitaka kujua kama serikali inatambua idadi kamili ya watoto wa mitaani wanaoishi kwenye mazingiara hatarishi.

“Tatizo la watoto waishio katika mazingira hatarishi linazidi kuwa janga la kitaifa nchini huku jitihada za kukabili likionekana kutopewa kipaumbele hali ni mbaya sana katika majiji makubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya ambapo idadi kubwa ya watoto hao hujihusisha na kuomba pamoja na matukio ya uhalifu ikiwemo wizi wa vifaa vya Magali wenye Maegesho.

“Je, serikali ina mpango gani wa kuanzisha kampeini ya kitaifa kukabiliana na tatizo hilo kwa nchi nzima ikiwemo kuwaweka kwenye vituo maalum na kuwapatia huduma za msingi.

Pia alitaka kujua kama serikali inatambua idadi kamili ya watoto wa mitaani wanaoishi kwenye mazingiara hatarishi” alihoji Mbunge huyo.

Dk. Ndungulile alisema kuwa serikali ina mpango wa kuwaunganisha watoto hao na familia zao na pale itakapobainika kuwa wazazi hawapatikani, watoto hao wataunganishwa katika familia za kuaminika wakati taratibu nyingine za kudumu zikiendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika, ikiwemo taratibu za malezi ya kambo, kuasili au kuwapeleka katika makao ya watoto.

Alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa mwongozo wa watambuzi wa watoto waio katika mazingira hatarishi na kuwaunganisha na huduma.

“Katika kipindi cha Julai 2017 hadi 2018 jumla ya watoto 864,496 ambapo wanaume ni 454,053 na wanawake ni 410,443 walitambuliwa kuwa wanaishi katika mazingira hatarishi katika mikoa yote nchini kasoro mikoa ya Lindi na Mtwara,” alisema Dk. Ndungulile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!