Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mjadala vifo vitokanavyo na mkaa, kuni washika kasi
Habari Mchanganyiko

Mjadala vifo vitokanavyo na mkaa, kuni washika kasi

Spread the love

MJADALA wa nishati ya kupikia kwa kutumia kuni na mkaa umezidi kushika kasi baada ya idadi kubwa ya Watanzania kujitokeza na kupiga simu bure ili kujisajili na kujiandaa na mjadala huo unaotarajiwa kufanyika Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Novemba mosi na 2 mwaka huu.

Katika mjadala huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumzia mjadala huo, Waziri Nishati, January Makamba, alisema zoezi linaloendelea sasa ni kuendelea na uelimishaji kuelekea kwenye mjadala huo unaosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote kwa ajili ya kuokoa idadi kubwa ya watu wanaopoteza maisha yao kutokana na sumu inayotokea kwenye kuni na mkaa wakati wote wanapoendelea na shughuli zao za mapishi katika majumba yao.

Alisema maoni yao yataambatana na hitaji la watu wanaotaka kushiriki mjadala huo kujisajili kwa kupiga namba ya bure 0800750203 au mtandao kwa www.cleancooking.co.tz kwa lengo la kuchukua maoni yatakayoboresha wazo la Watanzania kuondokana kwenye nishati ya kuni na mkaa na kuhamia katika gesi kwa gharama nafuu nchini kote.

“Hii nchi ni yetu wote na kila mmoja mmoja wetu anayo haki na wajibu wa kuboresha mambo haya ambayo serikali tunaamini idadi hii ya vifo vya akina mama wanaotumia kuni na mkaa kupikia itaondoka sambamba na kukuza uchumi wa kila mmoja.

“Nitoe rai sasa kila mtu mwenye nia ya kutoa maoni yake basi ajisajili kwa njia ya mtandao au kupiga simu ya bure apewe maelekezo kuelekea Novemba mosi na pili, huku tukio hilo likishuhudiwa na Rais wetu mpendwa, Samia Suluhu Hassan,” Alisema Makamba.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya afya, watu bilioni 2.4 duniani wanatumia nishati chafu zinazopelekea vifo vya watu bilioni 1.6, huku nchini Tanzania tukipoteza ndugu zetu wapatao 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!