Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mjadala sekta ya afya kufanyika Njombe
Afya

Mjadala sekta ya afya kufanyika Njombe

Spread the love

 

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Univeristy of Maryland Baltimore (UMB) kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Njombe imeandaa mjadala wa kitaifa wa kujadili jinsi ya kuboresha mfumo wa sekta ya afya nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Mjadala huo utafanyika tarehe 31 Machi 2022 mkoani Njombe, ikiwa ni siku mbili kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Mbio za Mwenye wa Taifa 2 Aprili 2022.

Akizungumzia lengo la mjadala huo, Mkurugenzi wa Ufundi wa UMB, Dk. John Kahemele ambaye pia ni Mdau wa Maendeleo Mkoa wa Njombe amesema, mjadala huo utahusisha watu mbalimbali wa ndani na nje ya mkoa huo.

Dk. Kahemele amesema, maendeleo yanategemea afya za wananchi na wao kama wadau wameona ni bora kuwakutanisha wadau na kujadiliana masuala kadhaa kisha kuwasilisha kwa kamati ya kitaifa ya maafa maoni na michango itakayotolewa.

“Tukipata maendeleo leo, lazima wananchi wake wawe na afya na sisi kama wadau tunafanya kazi na serikali kwa karibu kuona wapi tunaweza kusaidia. Sasa kwa kuwa Njombe kunafanyika uzinduzi wa Mbio za Mwenye 2 Aprili, tunatumia fursa hii kuwakutanisha wadau ili kujadili masuala ya afya,” amesema Dk. Kahemela.

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru

“Kuanzisha mjadala wa Kitaifa ambao tutaufanya Njombe jinsi gani mfumo wa afya unaweza kujipanga kukabiliana na majanga mbalimbali kama hili la UVIKO-19. Hatutaki uwe na bima ya afya ambayo hauwezi kutibiwa UVIKO-19, kwani haupo kwenye mfumo ulioorodheshwa, sasa kwenye mjadala tutaona nini kifanyike,” amesema

Aidha, amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kuchanjwa ili kujikinga na maambukizi, “na sisi tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu chanjo kwani kabla yah apo tuliona hali ilivyokuwa.”

Dk. Kihemela amesema, kabla ya uzinduzi wa mbio hizo kutafanyika maonesho mbalimbali ya wafanyabiashara na elimu za kujikinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI itatolewa.

Kuhusu uzinduzi huo wa Mbio za Mwenge, Dk. Kahemele amesema, “huu ni mwaka wa 10 kwa Njombe tangu kuanzishwa kuwa mkoa. Kuzindua Mbio za Mwenge ni jambo kubwa. Linafungua fursa mbalimbali za kimaendeleo na sisi wadau wa maendeleo tumeona tukafanye jambo Njombe.”

Amewaomba wakazi wa Njombe na mikoa jirani kujitokeza kwenye mjadala huo na elimu mbalimbali ambayo watakuwa wanaitoa juu ya kujikinga na magonjwa kadhaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga...

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

Afya

Asilimia 86 wenye umri zaidi ya miaka 18 wapata dozi kamili ya Uviko-19

Spread the love  KWA kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi...

error: Content is protected !!