May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mjadala Katiba mpya wawagawa wabunge

Bunge la Tanzania

Spread the love

 

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamegawanyika juu ya mchakato wa Katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Walikuwa wakichangia maazimio mawili leo Jumanne tarehe 30 Machi 2021, bungeni jijini Dodoma la kutambua mchango na kuenzi maisha ya Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Joseph Magufuli, na utumishi wake uliotukuka.

Pia, Azimio la Bunge la kumpongeza Samia Suluhu Hassan, kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk. Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum (asiye na chama), Sophia Mwakagenda amesema Rais Samia “anapaswa kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi mkuu.”

Sophia ambaye ni miongoni mwa wanachama 19 waliofukuzwa Chadema tarehe 17 Novemba 2020 kutokana na kukiuka miongozo ya chama kwa kwenda Dodoma kuapishwa amesema, Rais Samia anapaswa “aachilie wafungwa wote wa kisiasa.”

Amesema, kwa sababu Rais Samia alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba “kwa hiyo, aendelee na mchakato wa katiba mpya kwa kuanza na Rasmi ya Jaji Warioba.”

Ulipowadia wasaha wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Munde Tambwe kuchangia hoja hiyo amesema, aliyekuwa Rais Hayati Magufuli na makamu wake ambaye sasa ni Rais, wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana, hawakuahidi katiba mpya.

“Hawakuahidi Katiba mpya, msitake kumtoa Rais wetu kwenye reli. Hawawezi kutupangia, tutajipangia wenyewe. Rais aliwaahidi maendeleo na si katiba mpya.”

“Walitembea Tanzania nzima kuomba kura, wakiahidi maendeleo, zahanati, hawakuahidi Katiba mpya,” amesema Tambwe ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tambwe amesema, ana Imani kwamba, Rais Samia atatekelezwa vyema Ilani ya CCM yam waka 2020/25 “kwani narehemu na Rais walikuwa kama kulwa na dotto, kwa hiyo tutatekeleza.”

Kwa upande wake, Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo), Khatibu Said Haji amesema, suala la Katiba mpya si matakwa ya wabunge “ni matakwa ya Watanzania” kwa hiyo amemwomba Rais Samia kuhakikisha katiba mpya inapatikana.

 

 

Mara baada ya kauli hiyo, Mbunge Tambwe alisimama kutoa taarifa akisema, haelewi wanaohoji katiba mpya kwa sasa wakati wa Bunge Maalum la Katiba, walitoka ndani hivyo, hawakuona umuhimu wake na sasa wakae watulie wakati Serikali ikiendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Baada ya kauli hiyo, Khatibu alipewa fursa ya kuendelea na amesema “siwezi kupokea taarifa yake, kwani takwa la katiba mpya si la wabunge ni la Watanzania. Ndiyo maana ninyi mliipitisha hapa na mkashangilia.”

Khatibu amegusia suala la uhuru wa vyombo vya habari.

error: Content is protected !!