May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mjadala JPM kuongezewa muda uachwe huru – Butiku

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku

Spread the love

 

JOSEPH Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, ametaka mjadala wa Rais John Magufuli kuongezewa muda wa kutawala, uachwe huru. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mzee Butiku ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 6 Februari 2021, wakati akichangia mjadala wa uongozi ulioendeshwa katika Maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma.

Akizungumzia hoja hiyo, Mzee Butiku amewataka Watanzania kuwa huru kujadili suala hilo, huku akiwasisitiza wafuate taratibu.

“Watanzania tuwe huru kuzungumza mambo haya ya wakati, mkitaka kuamua mnafanya, lakini yasitupotezee umoja, sasa hivi maendeleo ya wananchi ni kipaumbele cha kwanza lakini tufuate taratibu,”

Mzee Butiku amesisitiza “hili la kutoka, kutotoka ni la utaratibu tu.  Mtu mmoja aliniuliza jana kuhusu mambo ya kung’atuka, nikasema ni mambo ya kuzungumza tu.

“Mbona Waingereza wazungu wameongoza miaka mingi, masultani haya wameendesha nchi zao miaka mingi, nani aliwauliza, waongo tu.”

Butiku alitoa kauli hiyo baada ya hoja hiyo kuibuliwa katika mjadala huo na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, aliyewataka Watanzania kupuuza taarifa za Rais Magufuli kuongezewa muda.

“Hivi karibuni kuna mjadala Katibu Mkuu (Dk. Bashiru Ally) amehangaika kuuzima, mwenyekiti amekataa (Rais Magufuli), ametutuma mara kadhaa tuwakumbushe wananchi kwamba ataheshimu Katiba,” amesema Polepole wakati akiendesha mjadala huo.

Mjadala huo uliibuliwa bungeni kufuatia baada ya mbunge wa Makambako CCM, Deo Sanga  kutaka Katiba ibadilishwe ili Rais Magufuli aongezewe muda wa kuongoza, kwa maelezo kwamba ameleta maendeleo kwa Watanzania.

Sanga alianzisha mjadala huo tarehe 3 Februari 2021 bungeni jijini Dodoma.

error: Content is protected !!