
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mizengo Pinda
MIZENGO Pinda, waziri mkuu wa Jamhuri, hafai urais. Hapaswi kufikiriwa kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaoweza kupendekezwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho. Anaandika Pendo Omary …(endelea).
Kinachomuondoa Pinda katika mbio za kusaka urais, ni kauli zake za kibabe dhidi ya wananchi; kushindwa kusimamia serikali na lundo la kashfa linalomkabili.
Waziri mmoja mwandamizi serikalini amesema, “ni hatari kwa taifa hili kukabidhiwa mwanasiasa anaina ya Mizengo Pinda.”
Amesema, “Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Pinda. Huyu bwana ameshindwa kusimamia serikali. Ni dhaifu anayetaka kuvitumia vyombo vya dola kulinda utawala wake.”
Akiongea kwa uchungu, waziri huyu amesema, “Tangu amekuwa waziri mkuu Pinda ameponyoka katika kashfa karibu nne huku walio chini yake wakitakiwa kujiuzulu.”
Kashfa ambazo Pinda amenyoka, huku mawaziri wake wakiangamizwa kisiasa, ni pamoa na ukwapuaji mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Escrow na operesheni tokomeza.
Pinda ndiye aliyeagiza jeshi la polisi kupiga raia kwa kile alichoita, “serikali imechoka kuvumilia.”
Kauli ya Pinda ni kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayopiga marufuku katika Ibara ya 12 kwa mtu yeyote kuteswa ama kuadhibiwa kinyama na kumpa adhabu, ambazo zinamtesa mtu na kumdhalilisha.
Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma 20 Juni 2013, “…umeambiwa usifanye hiki, wewe ukaamua kukaidi, utapigwa tu.”
Alikuwa akijibu swali la mmoja wa wabunge aliyetaka kujua “vitendo vya vyombo vya dola kupiga raia mkoani Mtwara.”
Alisema, “Ukifanya fujo, utapigwa tu. Maana hakuna namna nyingine. Maana lazima wote tukubaliane kwamba, nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.”
Alisema, “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiyo jeuri zaidi, watakupiga tu. Na mimi nasema muwapige tu. kwa sababu hakuna namna nyingine. Maana tumechoka sasa.”
Kuibuka kwa waziri huyo mwandamizi kudai Pinda amepoteza sifa ya kuwa rais; na kumtuhumu kuvitumia vyombo vya dola kulinda udhaifu wa serikali, kumekuja wiki moja tangu jeshi la polisi kumshambulia na kumdhalilisha mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba.
Prof. Lipumba alidhalilishwa wakati akielekea eneo la Zakhem, Mbagala, kuhutubia mkutano wa hadhara uliolenga kuwakumbuka mamia ya wafuasi na wanachama wa chama hicho, waliouawa na polisi Januari 26 na 27 mwaka 2001.
“Kama mtu amechoka kuongoza, huomba kupumzika. Kutumia vyombo vya dola kulinda udhaifu wako, ni kutaka kuingiza nchi katika machafuko. Hakukubariki,” ameeleza waziri huyo ambaye ameomba kutotajwa jina lake.
Pinda anatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa CCM walioamua kutafuta urais kufa au kupona.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema, Pinda siyo kwamba hakuhusika na kashifa ya Escrow, bali aliondolewa kutokana na kuwapo maridhiano.
“Wabunge wa CCM waliapa kutounga mkono mapendekezo ya Bunge. Waliweka sharti la kuondolewa Pinda. Walifanya hivyo ili kulinda serikali na Jakaya Rais Kikwete,” ameeleza Lissu.
Taarifa zinasema, wabunge hao wakiongozwa na Anne Kilango Malecela, walidai kuwa hawatapenda kumuona Rais Kikwete anakuwa na mawaziri wakuu watatu katika utawala wake wa miaka 10.
“Katika makubaliano hayo, ndipo unaona hata katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, naye anatolewa. Tuna ushahidi kwamba huyu bwana ndiye alikuwa anashinikiza fedha za Escrow kulipwa. Lakini tumeshindwa kumwajibisha kwa sababu ya tabia ya kulindana ya CCM,” ameeleza Lissu.
HILI NI JIPYA AMBAYO WASSIRA HANA BUDI KUPAMBANA NALO KAMA WAZIRI MPYA WA KILIMO NA USHIRIKA
Ufisadi mkubwa umeikumba shirika la taso kanda ya kaskazini huko arusha
kufuatia baadhi ya viongozi wake kudaiwa kutumia mali za taasisi hiyo
ya kilimo vibaya ikiwemo kuuza sehemu ay ardhi ambayo ilitengwa na
serikali kwa ajili ya kilimo darasa.
Habari kutoka ndani ya taasisi hiyo zinaeleza kuwa tayari baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa taso
kanda ya kaskazini na katibu wake wameuza sehemu ya ardhi ya taasisi
hiyo na kutuia fedha mifukoni mwao huku wanachama wakishangaa yale
yanayoendelea.
Vyanzo cha habari toka ndani ya chama hicho vinaeleza kuwa mwenyekiti na katibu wa taso
kanda ya kaskazini wamewauzia baadhi ya watu ardhi ya taasisi hiyo na
kugeuzwa kuwa maghala ya kuhifadhia mali ambazo haziendani na dhana
halisi ya taso ambayo ni kuendeleza kilimo kupitia maonyesho mbalimbali na kilimio darasa.
Cha kushangaza ni kuwa maeneo mengine yamegeuzwa kuwa magereji ya
kutengenezea magari tena kwa watu binafsi jambo ambalo linazidi kutia
hofu kuhusiana na uongozi wa taasisi hii ya kilimo.
Wanachama wa taasisi hii wamenza kuhoji ni kwanini matumizi halisi ya ardhi na viwanja vya taso
yanaendelea huku serikali ikiangalia wakati malalamiko mengi
yashawasilishwa katika ngazi mbalimbali ya kuwa hata utaratibu wa
ugawaji wa ardhi au viwanja vya taso arusha hakuzingatia kanuni ikwemo kuishirikisha bodi.
Wengi wanadai kuwa yote hayo yanatokana na uongozi wa chama hicho
kutokuwa na uhalali wa kuwa madarakani kwani hata mwenyekiti alieko
alirithi nafasi hiyo na hadi sasa hakuna uchaguzi uliofanywa kumweka
madarakani kihalali.
Tunachijuliza ni je taso taifa hawaoni
yote haya ynayotokea katika ofisi zake za kanda ya kaskazini? Waziri wa
kilimo chiza hajui kinachoendelea kweli? Je wakuu wa mikoa ya arusha, manyara na kilimanjaro ambao pia ni wahusika wakuu wa taso kanda ya kaskazini hajui kinachoendelea?
Ukweli ni kuwa wanajua kila kinachoendelea ila habari kutoka ndani ya
tasio zinaeleza wazi kuwa rushwa ndiyo chanzo cha yote hayo. Kuna habari
kuwa hata vyombo vya usalama vilivyotumwa kwenda kupeleka taarifa
kuhusiana na ufisadi uliokio ndani ya taso vimefika na kuona kila kinachoendelea lakini baada ya kupewa rushwa wananymaza kimya.
Taarifa zinaeleza kuwa mwenyekiti na katibu wa taso kanda ya kaskazini hawana kazi nyingine zaidi ya ikufuja mali za taasisi hiyo kiasi cha kuzifanya mali hizo ni zao binafsi.
Tayari kuna tuhuma ya kuwa wamekuwa akiuza sehemu ya ardhi na viwanja vya taso arusha
kwa watu binafsi ambao wamevigeuza kuwa maghala tena ya baadhi ya vitu
ambavyo haviendani na kilimo, je hii ndiyo kilimo kwanza?
Taarifa zinasema viwanja hivyo viletolewa kwa kati ya shilingi milioni
50 hadi milioni 100 na fedha hizo kutumika kuwahonga viongozi
mbalimbali kama vile wakuku wa mikoa na waziri wa kilimo na chakula bw.
Chiza ili kuficha yle yanayoendelea.
Mzozo wa hivi karibuni ni ule unasema kuwa katibu wa taso
kanda ya kaskazini na mwenyekiti wake walichukua shilingi milioni 60
kutoka kwa baadhi ya wale waliokodisha au kuuziwa viwanja pale arusha
kwa madai kuwa walikuwa wanawapelekea wakubwa akiwemo waziri wa kilimo
chiza lakini wahusika wakpata taarifa zimeishia mifukoni kwa wakubwa hao
jambo ambalo limezua tafrani kubwa kwa baadhi ya wanachama ambao
wanadai hajui chochote kuhusiana na michango hiyo.
Habari zinaeleza kuwa michango hii huwa inachangishwa mara kwa mara
kwa madai ya kuwa inawapooza wakubwa au kwenda kufadhili maswala
yanayohusiana na chama hicho wakati hakuna kinachoendelea
Kuna hanari zianeleza kuwa hata hati ya taso arusha
haijulikani iliko na kwamba kuna baadhi ya vuiongozi wameitumia kukopea
fedha kwa kisngizio cha kujenga kitega uchumi lakini wamezitumia
wenyewe.
Inasemekana kuwa wale wote wanaofuatilai swala la taso arusha
wamekuwa wakitishiwa maisha wakiwemo waandishi wa habari kiasi cha
kunyamaza kimya huku mali za taifa zifujwa hivyo wengi wamtoa rai ya
kuwa kama waziri ameshindwa kushughulikia swala hilo rais kikwete
mwenyewe alivalie njuga ili mali ya serikali isiendelee kutumiwa vibaya.
Wanasema waizri chizahataweza kwa vile ni mzigo na ccm yenyewe
imeshakiri hivyo kupitia mikutano iliyofanywa na katibu mkuu kinana
pamoja na nape nnauye kila walikopita.
Baadhi ay udhaifu wa waziri chiza wanasema ni aple aliposhindwa
kusimamia mali za kncu na tccco zisiuzwe lakini zikauzwa huku kukiwa na
madai kuwa kncu walimpa shilingi milioni 20 kwa ajili ya matengenezo ay
shule yake binafsi huko moshi.
Wanasema hafai kunedelea kuwa waziri wa serikali ya kikwete wakati
ametoa agizo kwa barua yenye nembo ya serikalli mali za tccco zisiuzwe
lakini zikauzwa na yeye akakaa kimya.
Lingine wanasema ni pale anaposhidnwa kutetea wazalishaji wa sukari
hapa nchini kwa kuruhusu kuendelea kuingizwa sukari ya nje kisha natoa
tamko kuwa serikalil haijatoa kibali. Sasa wanauliza kama haijatoa
kibali inaingiaje nchini na jee viwanda vya hapa nchini vifungwe? Huyu
ni mzig, ampumzishwe.
Lingine wanasema ameshindwa kusimamia mazao yaliyovunwa kwa wingi
kuhifadhiwa kwa njia yoyote ile maana serikali ina kila uwezo, badala
yake anawaacha wahusika kwenye wizara yake kushirikiana na walanguzi
kuwadhulumu wakulima huku wakitumia fedha za serikali kusafiri nje ya
nchi na huku wakiacha chakula kilichovunwa kikioza.
Mimi naamini Pinda, Sumay, Zito, Slaa, Mbowe, Membe, Mbatia, Mingiro, na wengineo wengi kutoka Chama tawala na vyote vya upinzani wana uwezo na haki ya kugombea ngazi ya uraisi na nafasi yoyote ya uongozi Tanzania ili mradi anakidhi taratibu zote zilizowekwa na katiba ya nchi. Nashangaa sana mtu anaibukia vyombo vya habari na kutoa kashfa (Mwanahalisi) PINDA HAFAI KUGOMBEA URAISI. Naomba tuwekeana Mipaka kwani huyu mheshimiwa Pinda ameongoza Tanzania kama waziri mkuu muda mrefu sasa.