January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miundombinu yakwaza walemavu

Walemavu wakicheza mpira

Spread the love

WATU wenye ulemavu nchini, wameiomba Serikali na taasisi binafsi zinazotoa huduma za kijamii kuhakikisha wanaweka miundombinu rafiki itakayowawezesha kuzifikia huduma kwa urahisi. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Rai hiyo, imetolewa na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Arusha, Yunusi Urasa, akisema kumekua na tatizo la la kukosekana kwa miundombinu hiyo, hali inayowakwamisha kupata huduma muhimu.

Akizungumza katika semina watu wenye ulemavu iliyofanyika jijini hapa jana kuandaliwa na Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini, ameitaka serikali kuwakumbuka walemavu katika upangaji wa miji, ujenzi wa barabara na majengo ili waweze kufikia huduma.

Amependekeza kuwepo kwa dawati maalumu la kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu litakalowasaidia walemavu kupata huduma kwa urahisi.

“Mlemavu asiyeona akienda benki hawezi kutumia kadi ya ATM, ni rahisi kuibiwa akikutana na mtu ambaye si mwaminifu. Pengine zitengenezwe kadi ambazo wataweza kuzisoma. Lakini mashine hizo pia ziko juu na hivyo kuwa vigumu kwa lemavu wanaotambaa kuzitumia,”amesema.

Naye Katibu wa Chama cha Watu wenye ulemavu wa ngozi Arusha, Happiness Raphael, amesema kuwa wanashangazwa kuona mauaji ya albino yanaendelea huku mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa yakikaa kimya.

Mratibu wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini, Francis Mhina amesema wanafanya juhudi za kutoa elimu kwa walemavu juu ya haki zao za msingi na namna ambayo wanaweza kujikwamua kimaisha.

Amebainisha kuwa, changamoto kubwa inayowakabili ni uhaba wa fedha, hivyo kushindwa kuwafikia walemavu wengi ambao wako vijijini.

error: Content is protected !!