Spread the love

JUMLA ya watahiniwa 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 250 wanatarajia kuanza mitihani ya kumaliza kidato ya sita kesho Jumatatu tarehe 9 Mei, 2022 na kumaliza tarehe 27 Mei 2022.

Pia watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya stashahada na cheti. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Mei, 2022, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 95,955 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita, 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

“Kati ya hao wanaume ni 47,859 ni wavulana sawa na asilimia 55.96 na wasichana ni 37,672 sawa na asilimia 44.04,” amesema Dk Msonde.

“Watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 151 na kati yao 136 ni wenye uoni hafifu na 15 ni wasioona.”

Amesema kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,424 waliojisajili, wanaume ni 6,546 sawa na asilimia 62.80 na wanawake ni 3,878 sawa ana silimia 37.20 na asiyeona ni mmoja.

Akizungumzia mitihani ya ualimu, Dk. Msonde amesema jumla ya 9,60 wamesajiliwa kufanya mitihani ya kozi za ualimu ambapo kati yao 4,560 ni ngazi ya stashahada na 5,110 ni ngazi ya cheti.

Msonde amesema kati ya watahiniwa 4,560 wa ngazi ya sthashahada wqaliosajioliwa 2,960 sawa na asilimia 64.91 ni wanaume na 1,600 sawa na asilimia 35.09 ni wanawake.

Aidha, kati ya watahiniwa 5,110 wa ngazi ya cheti waliosajiliwa, 2,336 sawa na asilimia 45.71 ni wanaume na 2,774 sawa na asilimia 54.29 ni wanawake.

Dk Msonde amesema baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.

“Baraza linatumia nafasi hii kuwataka wamiliki wa shule wote kutambua kuwa shule ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyaji mitihani hii,” amesema Dk Msonde.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *