October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mitihani kidato cha sita kuanza kesho, Necta yatoa onyo

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Necta

Spread the love

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limewaonya wamiliki wa shuke kuingilia majukumu yanayotendeka ama kufanywa katika mitihami ya kidato cha sita na ualimu inayotarajiwa kuanza kufanyika kesho Jumatatu. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Mitihani hiyo itaanza kesho Jumatatu hadi tarehe 16 Juni 2020.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jumapili tarehe 28 Juni 2020, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde amesema, baraza hilo halitasita kuwachukulia hatua pale watakapodhibitika pasi na shaka mmiliki wa shule amevamia ama kuingilia majukumu ya msimamizi wa eneo la mtihani kwa lengo la kuhujumu mtihani.

“Tutanawakaa wamiiki wa shule kutambua, vituo vyote vya mitihani ni vituo maalum na hivyo kwasasa ni mali ya baraza la mitihani na hivyo wamiliki wa shule hawapaswi kuingilia yanayotendeka,” amesema Dk. Msonde

Amewataka wakuu hao kujiepusha na maeneo hayo ili kuondoa mtafaruku na mtihani ifanyike kwa amani na utulivu.

Dk. Msonde amesema, mitihani hiyo itafanyika kwa shule za sekondari 763, vituo vya watainiwa wa kujitegemea 239, na vyuo vya ualimu 85 vyote vikiwa bara na zanzibar.

“Jumla ya watainiwa 85,546 ndio kidato cha sita, wamesajiliwa kufanya mtihani huo wa kidato cha sita kwa mwaka 2020 kati yao watainiwa wa shule wapo 74,805 na wakujitegenea wapo 10,741,” amesema.

Kati ya watainiwa wa shule 74, 805 waliosajiliwa, wavulana wapo 42, 284 , sawa na asilimia 56.53 wasichana 32, 521 sawa na asilimia 43.47 huku watahiniwa wenye mahitaji maalum wapo 113 kati yao 72 wenye uono hafifu, 16 wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia na watatu ni wenye ulemavu wa akili.

Wanafunzi wa kidato cha sita walipokuwa wanafanya mtihani

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, wavulana ni 7,109 sawa na asilimia 66.19 na wanawake wapo 3,632 sawa na asilimia 33.81.

Watahiniwa wa kujitegemea wenye mahitaji maalum, wawili ni wenye uono hafifu na wasioona ni mmoja.

Aidha, kwenye mitihani ya ualimu watainiwa 8, 985 wamesajiliwa ambapo kati yao 3,268 wa stashahada na 5,717 ngazi ya cheti huku kati ya watainiwa wa stashahada watahiniwa 1996 sawa na asilimia 61.08 ni ni wanaume na 1,272 sawa na asilimia 38.92 ni wanawake.

Hata hivyo, kati ya watainiwa wa ngazi ya cheti, 2,729 sawa na asilimia 47.73 ni wanaume 2,988 sawa na 52.27 ni wanawake.

error: Content is protected !!