Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Miswada ya madini ‘kaa la moto’
Habari MchanganyikoTangulizi

Miswada ya madini ‘kaa la moto’

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love

MJADALA mkali umeibuka katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma siku ya leo wakati Kamati ya Bunge ya iliyoundwa na Spika Job Ndugai kujadili miswada mitatu ya ulinzi na raslimali za nchi ikipokea maoni ya Wadau, anaandika Dany Tibason.

Miswada hiyo iliyowasilishwa jana Bungeni ni ule wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali zenye upungufu  wa mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu  Masharti hasi  katika Mikataba ya Maliasili wa mwaka 2017 na Muswada  wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusina na Umiliki wa Maliasili  wa mwaka 2017.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Pius Msekwa chini ya Dotto Biteko Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ambapo waliohudhuria kikao hicho walikuwa ni mawaziri, wabunge na wadau mbalimbali ambao walipata nafasi ya kuchangia.

Dk. Rugemeleza Nshala, mkurugenzi mtendaji wa Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT), akitoa maoni yake amesema sheria inaunda kamisheni ya madini na kuondoa madaraka ya waziri kujadiliana kwenye mikataba lakini haisemi ni nani ambaye atajadili.

“Kama tunaona kuna tatizo kuwa na mikataba, kwanini tusifuate mfano wa Zambia na Afrika Kusini ambapo utaratibu wao unasema hakuna kujadiliana mambo ya mikataba, wameingiza kwenye sheria ambapo ukitaka leseni ya kuchimba madini omba leseni na masharti yake yatakuwa kwenye sheria.

“Afrika kusini walitaka kufanya kuwa na mikataba wakakataa kwamba mtu ataomba leseni na kukutana na masharti ya kisheria humo na sio kuingia mikataba, tuangalie uwezekano wa hicho kitu,” amesema.

Gerald Mturi, Mwakilishi kutoka Tanzania Chamber of Minerals, amehoji ni nani atakayewajibika kama utatokea upotevu wa mali za mwekezaji na kwamba mwekezaji na atafidiwaje. Pia ameshangazwa na hatua ya serikali kutaka migogoro itatuliwe kwenye mahakama za hapa nchini.

“Wawekezaji wa nje kwa utaratibu huo hauleti amani, suala hili linatakiwa kuangaliwa upya kwa kuwa tutawakimbiza wawekezaji,” amesema.

Amepinga kifungu 10(1)-(3) kinachosema kwamba serikali inaweza kuwa na asilimia 50 ya hisa kwenye mgodi na kampuni ikatakiwa kupelekea tena hisa 30 kwenye soko la hisa jambo ambalo litaifanya kampuni kubaki na asilimia 20.

“Tunapendekeza kipengele hicho mfikirie namna ya kukiondoa hasa cha upelekaji hisa asilimia 30 kwenye soko la hisa kwa kuwa kitakimbiza wawekezaji,” amesema Mturi.

Katika hali ya kushtua, Hussein Bashe Mbunge wa Nzega Mjini, alimtuhumu Mturi kuwa amehusika na kudhulumu fedha za tozo za ushuru katika Halmashauri ya Nzega, mkoani Tabora.

“Unasema tukiweka kila kitu katika sheria tutakimbiza wawekezaji lakini Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, ilisema kuwe na Service Levy ya asilimia 0.03 lakini wewe umeondoka Nzega bila ya kulipa.

“Umelipa Sh. 2 bilioni tu kwa hoja kwamba kulikuwa hakuna sheria ndogo. Ndiyo maana tunasema kila kitu sasa kiwekwe kwenye sheria.”

Kwa upande wake John Bina Rais wa Shirikisho la wachimba madini wadogo wadogo Tanzania, akitoa maoni kwa niaba ya wachimbaji wadogo wadogo amesema, “Katika Miswada yote mitatu hakuna sehemu inayohusu wachimbaji wadogo wadogo, lakini pia muda wa umiliki tunapewa miaka saba pekee hili nalo liangaliwe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!