November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miss Tz 2018 achomoza kinyang’anyiro ujumbe NEC-CCM

Queenelizabeth Makune

Spread the love

 

MISS Tanzania 2018 – Queenelizabeth Makune ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia Jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Makune ambaye ni mzaliwa wa Shinyanga na msomi wa ngazi ya shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam atachuana na vijana wengine 13 kuwania nafasi tatu za Umoja wa Vijana wa CCM Bara (UVCCM).

Aliwahi kushinda mashindano ya ulimbwende katika vyuo vikuu Afrika (Miss University Africa) lakini pia ni mwanzilishi wa kampeni ya ‘Twenzetu Kutalii’ kufuatia kuteuliwa kwake na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa Utalii wa ndani kwa miaka miwili kuanzia Mwaka 2018.

Makune alikuwa mrembo wa kwanza kupanda hadi kileleni mwa Mlima Kilimanjaro akiwa na wasanii. Pia alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za urais mwaka 2020 na kundi la ‘Mama ongea na Mwanao’.

error: Content is protected !!