February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Miss Tanzania 2017 apatikana ‘juu kwa juu’

Julitha Kabete, Miss Tanzania 2017 (katikati) baada ya kukabidhiwa bendera

Spread the love

KAMATI ya Miss Tanzania kwa mara ya kwanza imeshindwa kufanya mashindano ya kumtafuta mrembo wake kwa mwaka 2017, badala yake imeteua msichana bila kumshindanisha na wenzake ili aende kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia yanayotarajia kufanyika nchini China, anaandika Angela Willium.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Hashimu Lundenga wakati wa kumkabidhi bendera ya Tanzania mrembo Julitha Kabete.

Amesema walipofanya uteuzi huo walipeleka barua Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kupata baraka zake.

Ametaja moja ya sifa waliozoangali katika kumteua mrembo huyo, ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuelewa mambo ya kimataifa na nidhamu na nidhamu aliyoionesha wakati yupo kambini jijini Mwanza .

“Mashindano mwaka huu yamepata misukosuko ndiyo maana tulikuwa kimya kwa muda hivyo mwaka huu hatujafanya shindano la kumtafuta Miss Tanzania, tumeamua kumchagua mrembo Julitha Kabete kwenda kushiriki shindano la Mrembo wa Dunia kutokana na kuelewa mambo ya kitaifa na nidhamu aliyoionesha kambini pia ni msomi”.

Aidha, mwakilishi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habibu Msummy amesema kutokana na changamoto wanazo pata serikali bado ipo pamoja nao kwani walifanya michakato pale katiba ya shindano la Miss Tanzania ilipofungia na hadi katiba ilipo funguliwa.

error: Content is protected !!