Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Misri yawaapisha majaji 100 wanawake
Kimataifa

Misri yawaapisha majaji 100 wanawake

Spread the love

 

BARAZA kuu la Serikali ya Misri limewateua kwa mara ya kwanza wanawake 98 kuwa majaji katika baraza hilo hilo ambalo ni moja ya vyombo vikuu vya idara ya mahakama nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Majaji hao waliapishwa jana tarehe 19 Oktoba, 2021 mbele ya Jaji mkuu wa Baraza hilo, Mohammed Hossam el-Din katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu Cairo.

Hatua hiyo imekuja miezi kadhaa baada ya Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi kuwataka wanawake wajiunge na vyombo vikuu viwili vya mahakama – baraza na mashtaka ya umma.

Tangu kuanzishwa kwake mwake 1946, Baraza la serikali limekuwa likiwateua wanachama wa kiume pekee na kabla maamuzi yaliyofanyika sasa.

Katika miaka iliyopita, wanawake walipinga maamuzi ya baraza, hilo wakisema kuwa wanabaguliwa.

Baada ya kuapishwa, mmoja wa majaji hao Radwa Helmy alisema hatua hiyo ilikuwa ni ndoto kwa wanawake wote nchini humo kwa kuwa nafasi waliyopewa ni mojawapo ya nafasi ya kipekee katika chombo kikubwa cha maamuzi nchini humo.

“Hili ni tukio la kihistoria, ni kama ndoto lakini sasa imetimia, kwa sababu chombo hicho kuwa na majaji wanawake tena kwenye nchi za kiarabu sio jambo dogo, tunamshukuru Mungu kwa hatua hii,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!