August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Misri, Nigeria zaishusha pumzi Stars

Spread the love

SARE waliyoipata Nigeria na Misri imepunguza presha ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2017 (AFCON)zilizopangwa kufanyika nchini Gabon, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Mchezo huo wa kundi G uliochezwa nchini Nigeria ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, na kuifanya Misri ibaki kileleni ikiwa na pointi saba, ikifuatiwa na Nigeria pointi tano na Stars itashika nafasi ya tatu ikiwa pointi nne, huku Chad ikiburuza mkia.

Kwa matokeo hayo, Stars itajiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu endapo itatumia vizuri michezo yake mitatu iliyobaki ikizingatiwa michezo miwili itacheza nyumbani dhidi ya Chad na Misri na mmoja utachezwa ugenini dhidi ya Nigeria.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo wake wa Jumatatu dhidi ya Chad huku ikiombea sare nyingine wakati Misri na Nigeria watakaporudiana Jumanne ijayo, ili wapande mpaka nafasi ya pili na kuishusha Nigeria nafasi ya tatu.

error: Content is protected !!