Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Misitu hatarini kutoweka nchini
Habari Mchanganyiko

Misitu hatarini kutoweka nchini

Spread the love

 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack amesema iwapo hakutakuwa na hatua madhubuti katika utunzaji na uhifadhi wa mitisu nchini ifikapo 2030 asilimia 47 ya msitu nchini itatoweka. Anaripoti Faki Sosi, Dodoma … (endelea).

Meshack amesema hayo juzi jijini Dodoma wakati akiwasilisha mada kwenye warsha ya wadau uhifadhi wa misitu kwa njia endelevu.

Amesema tafiti zinaonesha kasi ya uvunaji misitu imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, hivyo umefikia wakati muafaka kwa wadau kukaa na kujadiliana namna ya kukabiliana kasi hiyo, hali ambayo itawezesha kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Takwimu zinaonyesha kila mwaka hekta 469,000 za misitu huteketezwa kutokana na shughuli za binaadamu, ambapo utafiti unaonyesha asilimia 89 ya uvunaji wa misitu inatokana na kilimo , mkaa asilimia 7, mifugo asilimia 3,” amesema Meshack.

Mkurugenzi huyo amesema kwa mujibu wa takwimu hizo, hekta 469,000 zinazoteketea kwa mwaka ni sawa na ukubwa wa Mkoa Dar es Salaam, jambo ambalo sio la kufumbia macho.

Meshack amesema takwimu hizo za eneo la misitu yenye ukubwa wa jiji la Dar es Salaam kupotea kwa mwaka ni za 2017, hivyo inawezekana kiwango kikaqwa kimeongezeka katika kipindi cha miaka mitano sasa.

Amesema Serikali na wadau wa uhifadhi na mazingira wanapaswa kushirikiana kuhakikisha misitu inatunzwa na kulindwa kutokana na ukweli kuwa, rasilimali hiyo ni muhimu kiuchumi, kijamii na maendeleo.

Amesema TFCG na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), kupitia Mradi wa Mkaa Endelevu (TTCS), uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) wameona matokeo chanya iwapo jamii itashirikishwa katika kuhifadhi na kutunza misitu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack

“Wananchi wanaona fahari kulinda rasilimali zao kutokana na kushirikishwa, hasa wanapofaidika kwenye mapato binafsi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa zahanati, shule, ofisi, barabara, maabara na vinginevyo,” amesema.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa Serikali kutumia mradi huo wa mkaa endelevu ambao umetekelezwa kwenye vijiji zaidi ya 30, kusambaza kwenye vijiji vingine ambavyo vina misitu ya asili.

Meshack amesema iwapo kila mwananchi atashiriki katika uhifadhi na utunzaji rasilimali misitu, mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yatafanikiwa.

Ofisa Maliasili wa Mkoa wa Morogoro, Joseph Chuwa amesema mradi wa mkaa endelevu ambao umetekelezwa kwenye Halmashauri za Kilosa , Mvomero, na Morogoro umechochea maendeleo katika vijiji husika.

“Vijiji takribani 30 vya mkoa huu vimenufaika na TTCS, hasa kwa kupata huduma za kijamii kama zahanati, bima ya afya, nyumba za walimu, shule, kilimo, uchumi kukuwa na kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia,” amesema

Chuwa amesema mkoa umejipanga kuendeleza miradi ambayo imeibuliwa na TTCS, ili kuhakikisha jamii inaishi katika maisha bora na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyukim, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deusdedit Bwoyo amesema Serikali imejipanga kuhakikisha usimamizi shirikishi wa misitu inatekelezwa kila kona ya nchi.

Amesema ushiriki wa wananchi katika uhifadhi na utunzaji wa misitu utasaidia kuokoa rasilimali hiyo muhimu katika kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Bwoyo amesema Serikali imeanda sera na sheria kwa ajili ya uhifadhi na usimamizi wa misitu ambayo iliwashirikisha wadau wa sekta hiyo.

“Tupo katika hatua nzuri ya utunzaji wa misitu, kwani tumeandaa sera na sheria ambayo inawapa nafasi wananchi kushiriki moja kwa moja,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!