
David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi
KAMANDA wa POLISI mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, David Misime (SACP) amewataka wananchi kusitisha safari za kwenda Dodoma kama hawana shughuli za msingi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Misime ametoa kauli hiyo kufuatia mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Mkoani hapo ili wasiokuwa na shughuli maalum kuepukana na usumbuka kutoka na mkutano huo.
Aidha, mkutano huo utajumuisha viongozi wengi wa kitaifa na wajumbe wengi, hivyo kutokana na unyeti huo mawazo na masikio ya watu wengi nchi yataelekea huko ili kujua kinachoendelea.
Misime ameeleza, kwa kuwa mkutano huo utakusanya watu wengi, Jeshi la polisi Mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vya dola vingine wataimarisha ulinzi katika Mkoa huo ili wageni na wenyeji waweze kufanya shughuli zao kwa amani.
“Tutahakikisha amani na usalama vinakuwepo, pamoja na mambo mengine ikiwa ni pamoja na doria za miguu, magari, pikipiki, mbwa na farasi” amesema Misime.
Ameeleza, ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi kwa ufanisi, “tunaomba wananchi wa Dodoma na wageni mtupe ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbali pale mnapoona watu au mtu anafanya jambo lolote linaloashiria uhalifu ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa”.
Aidha, amewataka wamiliki na wahudumu wa nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi wa maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuwashauri na kuifadhi mali za wateja wao, na kutoa taarifa haraka kwa polisi waonapo kunadosari.
“Nitoe onyo kwa wale wenye mawazo ya kupanga kufanya uhalifu wa aina yoyote ile uwe wa kijinai au usalama barabarani atambue atashughulikiwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi” amesema Misime.
Ameongeza, “kunawengine wanaweza kuja tu kwa lengo la kuja kushuhudia kinachoendelea au kwaajili ya ushabiki nawashauri wasije kabisa ili kuepusha usumbufu na msongamano wa watu”.
More Stories
ACT-Wazalendo yasema bei ya vyakula imepaa, yatoa mapendekezo
CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika