TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), imefanya uchaguzi wa viongozi wake, pamoja na kuhamishia makao makuu ya kanda nchini Zimbabwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wenyeviti na Wakurugenzi wa MISA katika nchi tisa mwishoni mwa wiki iliyopita, walikubaliana kuhamishia makamo makuu nchini humo kutoka Zambia iliongoza tangu mwaka 2018.
Aidha, katika kikao cha bodi inayoundwa na wenyeviti wa nchi tisa za Kusini Mwa Afrika, alichagua Mwenyekiti wa MISA, Golden Maunganidze (Mwenyekiti MISA Zimbabwe), Makamu Mwenyekiti, Nkoale Ts’oana Joseph (Mwenyekiti MISA Lesotho) na Mwekahazina, Salome Kitomari (Mwenyekiti MISA Tanzania).
Maunganidze anachukua nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa MISA Zambia, Hellen Mwale tangu mwaka 2018.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti Mpya alisema “Hii ni fursa nzuri kwa MISA kufafanua na kutengeneza mikakati tuliyojiwekea ambayo itaimarisha msimamo wa uongozi kikanda juu ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.”
MISA ilianzishwa mwaka 1996 inaundwa na nchi za Tanzania, Malawi, Zambia, Msumbuji, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Eswatin, Namibia, Afrika Kusini na Angola ikiwa ni kati ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na jukumu lake kuu ni uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.
Leave a comment