May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Misa-Tanzania yabainisha changamoto 5

Mwenyekiti wa Misa-Tanzania, Salome Kitomari

Spread the love

 

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa-Tanzania) limebainisha changamoto tano zinazokwaza tasnia ya habari nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Changamoto hizo zimebainishwa leo Jumanne, tarehe 3 Mei 2020 siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo kwa Bara la Afrika inafanyikia jijini Arusha nchini Tanzania ikiwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti” huku mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Misa-Tanzania, Salome Kitomari amesema malengo ya kuwepo kwa Misa Tanzania ni kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa unakuwepo.

Amesema ukuaji wa vyombo vya habari imara vinavyowajibika na mazingira mazuri ya uandishi wa habari katika nchi wanachama kwa maendeleo na ustawi wa nchi zetu.

Pia, kuhakikisha umma unapata taarifa,na ndiyo maana kila Septamba katika right to know Day MISA Tanzania hutoa kufuli kwa taasisi za umma ambao zilifungia taarifa na funguo kwa zilizofungulia taarifa/

Amesema hii hufanyika kwa utafiti kwa kupeleka maombi ya taarifa kama mwananchi wa kawaida kwenye ofisi husika, kuwaandikia barua pepe zilizowekwa hadharani kwenye tovuti, kuwapigia simu kwa namba walizoweka kwenye tovuti, lengo ni kuona namna gani mwananchi wa kawaida kabisa anapata taarifa za maendeleo kwa urahisi na kuongeza uwajibikaji kwenye kutoa taarifa kwa taasisi za umma.

Salome amebainisha changamoto kuwa ni “baadhi ya sheria kuwa kitanzi kwa vyombo vya habari (Tunashukuru hili limeanza kufanyiwa kazi, tunatarajia mabadiliko ya sheria).”

“Hali duni ya maisha kwa waandishi wa habari kutokana na vyombo vingi kushindwa kulipa mishahara kwa wakati au kutolipa kabisa, kwa sababu mbalimbali ikiwamo hali ngumu ya biashara,” amesema.

Tatu ni, ushindani usio sawa kwenye matangazo kwa vyombo vya masafa ya ndani na vile vya nje, unaochangia kupunguza mapato kwa vyombo vya ndani ambavyo vimeajiri wengi, kukosekana utaratibu mzuri utaongeza changamoto ya ajira na kulipa wanahabari,pia ipo changamoto ya kodi ambayo ni kilio cha wamiliki wa vyombo vya habari.

Salome amesema jambo la nne ni ukuaji wa tekonolojia ulioleta ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni ambavyo vingi maudhui yake haifuati matakwa ya taaluma ya uandishi wa habari.

Na mwisho ni wananchi kutumia uhuru wao wa kujieleza mitandaoni (Citizen journalism) ambao wakati mwingine unafananishwa na taaluma ya habari kiasi cha wengi kushindwa kutofautisha na kujiita wanataaluma licha ya kutokuwa na vigezo.

“Lakini baadhi wananchi kutumia maudhui hiyo (inayorushwa na wananchi) kuhukumu waandishi wa habari wote kuwa hawajui matakwa ya taaluma yao,” amesema.

Aidha, Salome amesema “tunatarajia serikali yako itaendelea kusaidia ukuaji wa sekta ya habari,ikiwamo kuendelea kujenga mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara au waliowekeza kwenye vyombo vya habari ili waweze kutoa maslahi mazuri kwa wanahabari.”

error: Content is protected !!