Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Miradi ya uwekezaji yapungua kwa miaka mitano- CAG
Habari za Siasa

Miradi ya uwekezaji yapungua kwa miaka mitano- CAG

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Spread the love

 

CHARLES Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesema miradi mipya inayosajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), imepungua kwa asilimia 48, katika kipindi cha miaka mitano mfululizo (2015/16 hadi 2019/20). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

CAG Kichere ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi tarehe 8 Aprili 2021, wakati anatoa muhtasari wa taarifa ya ukaguzi kwa mwaka 2019/2020, jijini Dodoma.

“Katika mapitio yangu ya taarifa za mwaka na kanzi data ya wawekezaji katika TIC, nilibaini kushuka kwa idadi ya miradi inayosajiliwa na TIC, kwenye kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015/16 mpaka mwaka 2019/20,” amesema CAG Kichere.

Mkaguzi huyo wa hesabu za Serikali amesema, miradi hiyo imepungua kutoka 420 iliyosajiliwa TIC mwaka 2015/16 hadi kufikia 219 mwaka 2019/2020.

Wakati huo huo, CAG Kichere amesema, katika kipindi hiko, kiasi cha mitaji na nafasi za kazi zinazotokana na uwekezezaji, zilishuka.

“Pamoja na kushuka kwa idadi ya miradi, pia nilibaini kushuka kwa kiasi cha mitaji pamoja na idadi ya nafasi za kazi zinazotokana na uwekezaji,” amesema CAG Kichere.

CAG Kichere amesema, changamoto hizo zimesababishwa na mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya 2015, ambayo iliondoa baadhi ya vivutio vya kodi kwa wawekezaji.

“Kupungua kwa idadi ya miradi mipya pamoja na mambo mengine, kunatokana na mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2015 ambayo iliondoa baadhi ya vivutio vya kodi kwa wawekezaji.”

“Kwa mfano kuondoa vivutio vya kodi katika upanuzi wa miradi kutoka katika kundi la miradi inayopaswa kupewa vivutio vya kodi,” amesema CAG Kichere.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Amesema kushuka kwa idadi ya uwekezaji kuna athari kubwa kwa Taifa, kwani kunapunguza fursa ya ajira, kodi, ujuzi pamoja na usambazaji wa Teknolojia.

Taarifa hiyo ya CAG Kichere imekuja siku mbili tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuiagiza Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Akizungumza katika hafla ya uapisho wa viongozi katika Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Aprili 2021, Rais Samia aliagiza wizara hiyo iboreshe taratibu za utoaji vibali na viwango vya utozaji kodi, ili kuwavutia wawekezaji wapya na waliokimbia nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!