Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Miradi kichefuchefu inayoitia doa Serikali Kinondoni
Makala & UchambuziTangulizi

Miradi kichefuchefu inayoitia doa Serikali Kinondoni

Spread the love

UKIMYA na usiri umeendelea kutawala kuhusu kukwama kwa miradi mitatu ya Halmashauri ya Kinondoni inayogharamiwa kwa vyanzo vya mapato ya ndani na kuitia doa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Miradi hiyo ni ile ya ujenzi wa Stendi ya Mwenge kwa gharama ya Sh 4.8 bilioni, jengo la ofisi za Manispaa ya Kinondoni Sh 2 bilioni na ujenzi wa uwanja wa mpira wa klabu ya Kinondoni (KMC).

Miradi hiyo ilianza kutekelezwa Aprili 2020 na Mkandarasi 361 JWT Lugalo na ilipaswa kukamilika tarehe 20 Mei 2021 kwa utaratibu wa ‘Force Account’ ambapo halmashauri inanunua vifaa na mkandarasi anajenga.

Licha ya miradi hiyo kufuatiliwa na viongozi wa juu wa Serikali kwa maana ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Katibu Mkuu, Mkuu wa mkoa, Mkurugenzi wa Manispaa na Mkuu wa Wilaya, lakini hadi sasa miradi hiyo imesimama na hakuna taarifa yeyote.

Tarehe 20 Juni 2021 aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu alitembelea mradi wa stendi ya magari Mwenge na kukuta umefikia asilimia 46 tu huku kiasi cha Sh 1.558 bilioni kikiwa kimeshatumika.

Waziri Mwalimu, alisimamisha miradi yote mitatu kuanzia tarehe 20 Juni 2021 baada ya kuona inasuasua na kumuagiza Katibu Mkuu wake kuunda timu huru ya uchunguzi.
Timu ya uchunguzi ilipewa wiki mbili kuanzia tarehe 20 Juni 2021 kukamilisha kazi hiyo na kumkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi.

Timu hiyo ilipaswa kukamilisha kazi yake tarehe 4 Julai 2021, lakini leo hii ni miezi minane hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ujenzi umesimama kwa kipindi hicho chote.

Mara ya mwisho taarifa kuhusu mradi huo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa, Amos Makala, alipofanya ziara ya kuitembelea tarehe 30 Oktoba 2021 ambapo aliwahakikishia Wanakinondoni kuwa ujenzi ungeendelea wakati wowote kuanzia siku hiyo kwani angetoa barua ya kuelekeza kuendelea kwa miradi hiyo.

Makala alidokeza siku hiyo kuwa amejiridhisha kuwa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya uchunguzi na hatua alizochukuwa Waziri Ummy Mwalimu zilikuwa sahihi.

Makala alisema atasimama kidete kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ubora lakini hadi leo tarehe 31 Machi 2022 ni miezi mitatu imepita tangu atoe kauli hiyo na hakuna kilichoendelea kwenye miradi hiyo.

Tangu wiki iliyopita, MwanaHALISI Online imekuwa ikiwatafuta viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam wakiwamo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, ambao kwa nyakati tofauti simu zao ziliita bila kupokewa na walipotumia jumbe fupi za maneno hawakujibu chochote.

MwanaHALISI ilimtafuta pia Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa bila mafanikio baada ya simu yake kuita bila kupokewa na alipoandikiwa ujeumbe mfupi wa maneno hakujibu chochote.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni wakati huo, Spora Liana, aliwahi kunukuliwa Wakati wa ziara ya Ummy Mwalimu kuwa; “Changamoto kubwa ni vifaa kutoagizwa kwa wakati, vibarua wachache, ambapo mkandarasi badala ya kutumia askari anaajiri raia, pamoja na kuchelewa kulipwa mishahara yao na kuja ofisi kwangu kunilalamikia,” alisema Liana.

Mkandarasi wa mradi huo, Luteni Kanali David Luoga, kwa upande wake alisema Aprili 2020 walianza kazi ya ujenzi wa stendi hiyo na kazi yao ni kujenga lakini vifaa vya ujenzi vinaletwa na Manispaa ya Kinondoni.

“Ilipofika Julai 2020, mtiririko wa vifaa haukuwa mzuri, vikawa vinakuja kwa kusuasua, ilipofika Septemba tuliandika barua ya kuomba vifaa vyote vinavyovihitaji kufika eneo la mradi lakini hadi sasa havijafika,” alisema Luteni Kanali Luoga.

1 Comment

  • It is true about these white elephant.problem here is that those responsible to take action and those who committed these crimes both protect each.There is doubt about that the public is suffering.But who cares?A military,non engineers,etc are engaged by the Govt .I have seen such a serious negligence of the highest order.I don’t know if any of TGWG can take measure against a President Commisioned Military officer.You need to investigate more to shed more light to the public.thanks.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!