May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Milioni moja wafariki dunia kwa corona

Spread the love

WAGONJWA milioni moja duniani wamefariki kutokana na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mtandao wa worldometer umeripoti leo Jumanne tarehe 29 Septemba 2020, waliopona kutokana na ugonjwa huo ni milioni 24.89 huku maambukizo yakifikia milioni 33.57.

Marekani imeendelea kuwa Taifa linaloongoza kwa maambukizo milioni 7.36, kati yao waliofariki dunia wakiwa 209,808 na waliopona virusi hivyo ni milioni 4.6.

India inafuatia ikiwa na maambukizo milioni 6.14, waliopona milioni 5.1 na waliofariki dunia 96,351. Brazil inashika nafasi ya tatu ikiwa na maambukizo milioni 4.74, waliofariki 142,161 na waliopona ugonjwa huo wakiwa milioni 4.

China ambako corona ilianzia mwishoni mwa mwaka 2019 ina maambukizo 85,384 na vifo vikiwa 4,634 na waliopona wakiwa 80,566

error: Content is protected !!