May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 91 wapona corona duniani

Spread the love

 

MAAMBUKIZO ya virusi vya corona (COVID-19), ulimwenguni yamefikia milioni 116.22 huku waliopona maambukizi hayo wakiwa milioni 91.89. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Waliofariki kutokana na maambukizo hayo hadi leo Ijumaa asubuhi tarehe 5 Machi 2021, ni milioni 2.58.

Marekani ndiyo Taifa ulimwenguni, linaongoza kwa kuwa na maambukizo mengi ambayo yamefikia milioni 29.52, waliofariki ni 533,636 huku waliopona wakiwa milioni 20.

India inafuatia ikiwa na maambukizo milioni 11.17, waliofariki 157,584 na waliopona milioni 10.83.

Brazil, inashika nafasi ya tatu ikiwa na maambukizo milioni 10.7, waliofariki 261,188 na waliopona maambukizo hayo wakiwa milioni 9.6.

error: Content is protected !!