October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 7 wapona corona duniani

Spread the love

WAGONJWA milioni 7.58 waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona (COVID-19) duniani wamepona. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa Worldometer, hadi kufikia leo asubuhi Jumatatu tarehe 13 Julai 2020, wagonjwa milioni 13.03 wameambukizwa corona duniani. Kati ya wagonjwa hao, waliofariki dunia ni 571,659.

Marekani imeendelea kuongoza kwa kuwa na maambukizo milioni 3.41, waliopona milioni 1.5 na waliofariki dunia 137,782.

China ambako corona ilianzia mwishoni mwa mwaka 2019, ina maambukizo 83,602 kati ya hayo, waliopona ni 78,648 na waliofariki dunia wakiwa 46,34.

error: Content is protected !!