May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 500 kuboresha hospitali wilaya Iringa

Hospitali ya Frelimo

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetenga Sh. 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto, wanaume na wanawake ya magonjwa mchanganyiko hospitali ya Frelimo ya wilaya ya Iringa. Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 21 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde akijibu swali la Ritta Kabati, Mbunge wa viti maalumu (CCM).

“Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanaume, akinamama na watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Frelimo katika Manispaa ya Iringa?”

Akijibu swali hilo, Silinde amesema, hospitali ya halmashauri ya manispaa ya Iringa (Frelimo), imeanza kufanya kazi kama Hospitali ya Halmashauri Februari 2012 na kusajiliwa rasmi mwaka 2013.

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Silinde amesema, mwaka wa fedha 2017/18, Serikali iliipatia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Sh.400 milioni, kwa ajili ya upanuzi wa hospitali ambapo jengo la maabara na jengo la mionzi yalijengwa na kukamilika.

“Miundombinu iliyopo katika Hospitali ya Frelimo ni pamoja na jengo la utawala, jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD), jengo la huduma za maabara, jengo la huduma za mionzi, jengo la kufulia na jengo la huduma za Afya ya uzazi na mtoto.

“Miundombinu inayokosekana katika hospitali hii ni pamoja na jengo la upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa, jengo la kuhifadhi maiti na jengo la kutunzia dawa.”

“Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imetenga Sh. 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto, wodi ya wanaume na wodi ya wanawake magonjwa mchanganyiko,” amesema Silinde.

error: Content is protected !!