
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiwa wanasimika nguzo za umeme
SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limetenga Sh. 43.46 milioni kwa ajili ya kuunganisha umeme katika kijiji cha Gurungu Wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini, Stephen Maselle- Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), kazi zilizofanywa ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33, umbali wa kilometa 0.5, ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 0.4 umbali kilomita 1 na kufunga trasfoma 1 ya kVA 50.
Hata hivyo, amesema kijiji cha Aghondi kimeingizwa katika mpango wa miradi inayofadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia mfuko wa MCC awamu ya II.
“Tunachosubiria ni hatua za upembuzi na athari za kimazingira kufanyika na wataalamu wa MCC ili mradi uingizwe katika utekelezaji,”alisema.
Maselle alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni, John Lwanji (CCM), ambaye alitaka kujua mpango wa kuunganisha umeme katika vijiji vya Aghondi, Mabondeni na Kitopeni umefikia wapi.
More Stories
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika
Mbivu, mbichi kesi ya kina Mdee kujulikana leo
Tunafuatilia miradi hatufanyi mikutano ya hadhara:CCM