May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 176 zawafikisha wawili kortini

Spread the love

WATU wawili wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa kuibia kampuni ya Dimond Motors zaidi ya Sh.176.2 milioni. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam .. (endelea).

Watuhumiwa hao ni Emmanuel Sabuni na Linda Mtengule ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Wamesomewa mashtaka yao leo Alhamisi tarehe 10 Desemba 2020 na Wakili wa Serikali, Yusuph Abood mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate.

Shtaka la kwanza, linalowakabili watuhumiwa hao ni pamoja na wizi wa vifaa vyenye thamani ya Sh.176.2 milioni

Shtaka la Pili, kugushi nyaraka ambapo inadaiwa watuhumiwa hao kati ya tarehe 1 Januari 2019, na 31 Desemba 2019, walighushi mihuri ya kampuni ya Mac Auto Accessories kwa lengo la kujipatia fedha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu

Shitaka la Tatu, ni kughushi nyaraka ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kati ya tarehe mosi Januari 2019, na 31 Desemba 2019 walighushi mihuri ya kampuni ya Degraglo Services Agency Ltd kwa lengo la kujipatia fedha.

Shtaka la mwisho, washtakiwa hao wanadaiwa kughushi nyaraka za kampuni ya Brand Tyres kwa lengo la kujipatia fedha.

Wakili Abood alipomaliza kusoma mashtaka hayo, washtakiwa walikana mashataka yao na kueleza kuwa upelelezi haujakamilika.

Hakimu Kabate aliwapa masharti ya dhamana kwa kutoa Sh.88 milioni, kudhaminiwa na mdhamini mmoja kwa kila mshatakiwa pamoja na kusaini bondi ya Sh.10 milioni shilingi

Washtakiwa hao, wamerejeshwa lumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana. Shauri hilo litatajwa tena tarehe 23 Desemba 2020.

error: Content is protected !!