Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Milioni 105 zanyakuliwa NMB Mastabata
Habari Mchanganyiko

Milioni 105 zanyakuliwa NMB Mastabata

Spread the love

DROO za kila wiki za kampeni ya NMB MastaBata-Kote Kote zimetamatika leo Ijumaa, tarehe 27 Januari 2023 baada ya zoezi la kuwapata washindi 76 wa mwisho kufanyika katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB la Wami. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Sasa imebaki droo moja ya kuwapata washindi wa zawadi ya kwanza ambayo ni safari ya mapumziko ya siku nne iliyolipiwa kila kitu huko Dubai itakayowahusisha wateja wanne pamoja na wenza wao.

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Wami, Harold Lambileki (katikati) akibonyeza kitufe kumtafuta mshindi wa pikipiki katika droo ya kumi na ya mwisho ya wiki ya NMB mastabata kote-kote katika Tawi la benki ya NMB Wami Manispaa ya Morogoro, jumla ya washindi 75 walijishindia pesa taslimu laki moja na mshindi mmoja kujinyakulia pikipiki aina ya Boxer. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Morogoro Business center na kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya Bahati na nasibu, Joram Mtafya.

Kwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamekuwa wakinyakua Sh100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.

Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na Sh75 milioni pesa taslimu kwa washindi 750 na Sh 30 milioni za Boxer 10. Jumla ni Sh105 milioni na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya Sh300milioni.

Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Bw Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Wami, Harold Lambileki (katikati) akibonyeza kitufe kumtafuta mshindi wa pikipiki katika droo ya kumi na ya mwisho ya wiki ya NMB mastabata kote-kote katika Tawi la benki ya NMB Wami Manispaa ya Morogoro, jumla ya washindi 75 walijishindia pesa taslimu laki moja na mshindi mmoja kujinyakulia pikipiki aina ya Boxer. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Morogoro Business center na kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya Bahati na nasibu, Joram Mtafya.

 

“Kampeni ya NMB MastaBata-Kote Kote imekuwa ni ya mafanikio makubwa sana. Baada ya droo hii ya leo, idadi ya washindi wa kila wiki itafikia 760 ambapo 750 ni wale wa Sh 100,000 kila mmoja na 10 wa pikipi,” Lambileki alibainisha. Sokoni thamani ya kila Boxer ni takribani Sh3 milioni.

Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na NMB Mastercard QR anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.

Mbali na kuhamasisha matumzi ya kadi za malipo za kidijitali za NMB, kampeni za MastaBata pia zimekuwa zikilenga kuwalipa fadhila wateja na kama sehemu ya kurudisha sehemu ya faida za NMB kwa jamii.

Zawadi za MastaBata-Kote Kote zilizingatia pia kuwawezesha washindi kiuchumi. Mbali na droo 10 za kila wiki, zilifanyika droo nyingine mbili za kila mwezi ambapo washindi 98 walishinda jumla ya Sh98 milioni na wanne piki piki.

Huu ni mwaka wa wanne wa mfululizo wa kampeni za NMB MastaBata kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard. Mchakato huu ulianza na MastaBata mwaka 2018, kisha MastaBata Sio Kawaida na baade MastaBata – KivyakoVyako na hii ya MastaBata-Kote Kote iliyoanza mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!