October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taratibu za kimila zatumika kutafuta wauaji

Maelfu ya wakati wa Karatu wakiwa katika mazishi ya Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Martin Goi (picha ndogo)

Spread the love

MAELFU ya wananchi wameshiriki katika mazishi ya Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Martin Goi, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na wanaoitwa na serikali, “watu wasiojulikana.” Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Goi alipigwa risasi tarehe 15 Januari mwaka huu, katika mgahawa wa Rhotian Glades, wilayani Karatu, majira ya saa tatu usiku. Goi alizaliwa katika kijiji cha Dofa wilayani Karatu.

Taarifa zinasema, mara baada ya shambulio hilo na kabla mauti kumfika, Goi alipelekwa kwenye hospitali ya Sanawati mkoani Arusha. Alifia katika hospitali hiyo siku mbili baada ya kushambuliwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, mara baada ya marehemu Goi kuzikwa, wananchi kadhaa walishiriki katika maombi maalum ya kumtambua waliofanya mauaji hayo.

Maombi hayo yalihitimishwa jana tarehe 22 Januari kwa dua na sala za kimila na kidini. Kwa kawaida, maombi ya aina hiyo hujibu katika kipindi kifupi cha wiki moja.

error: Content is protected !!