May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mil 5 zamtesa Joyce Kiria

Spread the love

JOYCE Kiria, Mwanaharakati wa masuala ya wanawake, anasaka Sh. 5 Mil ili kulipa faini baada ya kuweka maudhui mtandaoni bila kufuata sheria. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Mwanaharakati huyo, alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku nne kutokana na kuweka maudhui mtandaoni bila leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

Kiria anamiliki mtandao wa Wanawake Live, ambai huutumia kuweka vipindi mbalimbali kuhusu masuala ya ukatili kwa wanawake.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, ameiomba jamii kumsaidia kulipa fedha hizo, na kwamba hakufahamu kama maudhui ya aina hiyo yanahitaji usajili.

“Maudhui ambayo naweka ni ya kusaidia jamii, sikujua kama natakiwa niwe na leseni kwasababu najua maudhui yangu sio ya kibiashara, wakati naendelea na harakati zangu nilijua hayahitaji kuwa na leseni.

“..ni kweli kutojua sheria haikupi uhalali wa kutenda kosa, nilishikiliwa na jeshi la polisi kwa muda wa siku nne na sasa nipo nje kwa dhamana, natakiwa kulipa faini ya milioni 5 ambayo kiukweli hiyo hela mimi sina,” amesema.

Amesema, kupitia maudhui yake, hafanyi biashara na wakati mwingine anakua hana hata laki moja.

“Mimi ni mtu ambaye naweza kukosa hata laki moja, sifanyi biashara, naomba mnisaidie niweze kulipa faini na niendelee na harakati zangu.

“Nipo kwenye wakati mgumu sana, lakini kudondoka kupo au changamoto zipo kwenye maisha, hili limenitikisa kiasi chake”.

Kiria amewasihi watumiaji wengine wa mtandao huo nchini ambao hawajasajili kupitia TCRA, wajifunze kutoka kwake, kwamba wakakate leseni.

error: Content is protected !!