
Dk. Stephen Kebwe, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
SERIKALI mkoani Morogoro imetenga Sh. 36 milioni ilizobana wakati wa sherehe za Mwenge kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa maafa na dharura wa mkoa ili kusaidia waathirika wa mafuriko mwaka huu, anaandika Christina Raphael.
Dk. Stephen Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema hayo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya wauguzi zilizofanyika kimkoa na kuhusisha wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa Morogoro.
Amesema, tayari wamegawa misaada ya vyakula mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko katika wilaya zote za Morogoro ikiwemo Wilaya ya Morogoro Vijijini na kwamba, Wilaya ya Kilosa ndio pekee iliyobaki.
Dk. Kebwe almesema, fedha hizo zimetokana na michango mbalimbali ya wadau iliyotolewa wakati wa sherehe za mwenge kitaifa zilizofanyika mjini humo ambapo wameamua kuziingiza kwenye mfumo huo baada ya kubana bajeti ya Mwenge ili kusaidia waathirika mbalimbali.
Amesema, walilazimika kujipanga katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazowakabili kwenye mafuriko kufuatia Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kueleza mazingira ambayo nchi inaenda kukabiliana nayo.
More Stories
Wanafunzi walilia madarasa Mtwara, Silinde awajibu
LSF, NGO’s zajadili mfumo upatikanaji haki Tanzania
Majaliwa atoa maagizo kwa wazazi, walezi