Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mil 3.9 kujenga vyoo Morogoro
Habari Mchanganyiko

Mil 3.9 kujenga vyoo Morogoro

Spread the love

JUMLA ya Sh. 3.9 milioni zimekusanywa na wanavijiji wa vijiji vinne vya kata ya Tomondo wilayani Morogoro na kutatua tatizo la uhaba wa vyoo na vyumba vya kujistiria katika shule za msingi ili kunusuru kushuka kwa kiwango cha elimu hasa kwa mtoto wa kike. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Diwani wa kata hiyo, Hamisi Msangule amesema wameamua kujenga vyoo hivyo baada ya kufikia makubaliano kama kata ya kuwa na uhakika wa vyoo na vyumba vya kujistiria watoto wa kike ili kupunguza utoro na kuongeza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi wawapo shuleni.

Alisema, fedha hizo zimetolewa kwa nguvu za wananchi hao na kwamba mpaka sasa shule ya msingi kikundi tayari  imekamilisha ujenzi wa vyoo  kwa matundu sita kwa wasichana na sita kwa wavulana huku Mvuleni wakiwa wameshaanza ujenzi wa matundu sita ya vyoo ambayo ni vya nyongeza baada ya kupokea Sh. 66.6 milioni kutoka kwenye bajeti ya maendeleo ya kata kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3 na matundu sita ya vyoo.

Msangule alisema, shule ya msingi Lukonde ipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi wa matundu nane ya vyoo huku Kibungo Kungwe wakiwa wameshaanza ujenzi wa matundu sita ya vyoo ambayo yapo katika hatua za mwisho.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Jotham Sanga amethibitisha hilo na kusema, ujenzi wa vyoo na vyumba vya kujistiria watoto wa kike unaendelea kwenye kata hiyo huku shule zingine zikiwa zimeshakamilisha ujenzi huo na zingine zikiwa katika hatua tofauti.

Alisema, wanavijiji hao wameweza kukusanya kiasi cha Sh. 3.9 milioni na kuweza kujenga matundu hayo ya vyoo yanayotarajiwa kukamilika mapema mwaka huu ili kusaidia ukuaji wa kiwango cha elimu kwenye shule zilizopo katika kata hiyo.

Naye Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kikundi, Renatus Kisima alisema kwa sasa wanampango wa kuandaa vifaa kwa ajili ya kuwawekea watoto wa kike ili waweze kujistiri baada ya chumba chao kukamilika.

Alisema, chumba hicho kimeshakamilika na kwamba kinasubiria vifaa hivyo tuu ili kifunguliwe kwa ajili ya matumizi kwa wanafunzi wa kike ambao ndio walengwa.

Kisima alisema, watoto wa kike wamekuwa wakikumbwa na kushuka kwa kiwango cha taaluma kufuatia kila mwezi kupumzika nyumbani kwa siku zaidi ya moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!